Waziri wa nchi ofisi ya Rais Mhe.Prof.Mark J.Mwandosya akizungumza na Mawaziri wa Rwanda.Kutoka kulia ni waziri ofisi ya Rais Mhe.Venantie Tugireyezo, Waziri wa mambo ya nje Mhe.Louise Mushikiwabo pamoja na kaimu balozi wa Tanzania nchini Rwanda Bw. Francis Mwaipaja.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Mhe Prof. Mark Mwandosya akimkabidhi waziri wa mambo ya nje wa Rwanda Mhe. Louise Mushikiwabo ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete kwenda kwa Rais wa Rwanda Mhe.Paul Kagame.kulia ni Waziri Ofisi ya Rais Mhe. Venantie Tugireyezo

Waziri wa nchi ofisi ya Rais Mhe. Prof. Mark J. Mwandosya akimkabidhi kitabu alichoandika kuhusu udhibiti wa huduma za kiuchumi nchini Tanzania Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda Mhe. Louise Mushikiwabo. Anayeshuhudia ni Waziri Ofisi ya Rais Mhe. Venantie Tugireyezo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hongera sana Mhe. JK, Kwani hatua hii ya kumruhusu Mhe. WZR wako kufanya ziara Rwanda ni ishara tosha kwamba Watanzania hatuna chuki dhidi ya jirani zetu wa Rwanda, tunawapenda na tunauenzi ushirikiano wetu na Rwanda.

    Historia ya ulimwengu, inaonyesha kuwa Watanzania siku zote tumekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha amani kwa majirani zetu na pia kwa ulimwenguni kote.

    Mungu ibariki Tanzania.
    Mungu ibariki Afrika


    ReplyDelete
  2. This "open hand policy " itawaacha wenzetu bila sababu nyingine zaidi ya wao pia kufunguka na kuuambia ulimwengu "kunani" Asante sana Rais wetu.

    ReplyDelete
  3. Hii ni Tiba tosha!

    Hakukuwa na sababu ya kufuga mawazo ya sintofahamu kwa ndugu zetu wa Rwanda dhidi yetu Tanzania.

    Ni bora mzizi wa fitina umekatwa na sasa Tanzania na Rwanda tufungue ukurasa mpya wa maisha tuishi kwa kuaminiana bila kuhisiana vibaya na kuishi kwa kuogopana na kutuhumiana mwisho wake sio mzuri!!!

    Ahsanteni sana Serikali.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...