Spika wa Bunge Mhe. Anna Makinda akijaribu mojawapo ya viti vipya vilivyofungwa katika ukumbi wa Bunge tayari kwa ajiri ya Matumizi wakati wa Bunge la Katiba. Mhe. Makinda aliongoza ujumbe wa Tume ya Utumishi wa Bnge kufanya ukaguzi wa mwisho kabla ukumbi huo haujakabidhiwa kwa Sekretariat ya Bunge la Katiba Jumatano wiki hii.
Spika wa Bunge Mhe. Anna Makinda akiwa na wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge kukagua ukumbi huo.
Spika wa Bunge Mhe. Anna Makinda, (katikati) Naibu Spika Mhe. Job Ndugai (kushoto), Katibu wa Bunge (Wa pili Kulia) na Mhe. Hamadi Rashid Mohamed Kulia wakiangalia baadhi ya maboresho yaliyofanywa katika Ukumbi wa Bunge kwa ajili ya Bunge la Katiba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hivi ni kwanini hili Bunge la Katiba halikupangiwa kukaa Dar kwenye ukumbi mpya wa Mwl Nyerere ambao tayari ungeweza kuchukua hao wabunge wote 600?. Sasa hapo Dodoma baada ya hilo bunge kumaliza hizo siku 90 itakuwaje?. Moja ya mapendekezo ya ra rasimu ya katiba mpya ni kuwa idadi ya wabunge iwe 70 sasa kwenye ukumbi wenye viti 600 itakuwaje?

    ReplyDelete
  2. Mbona viti mmevifanya vidogo? Baadhi ya mapandikizi ya watu yataenea kweli?? Kwa maoni yangu kuna baadhi ya viti mngeviaji kama vilivyokuwa awali kulingana na idadi ya mabonge yatakayokuwa kwenye bunge la katiba. Pia kwa hizo seats watu watabanana. Nashauri wanawake na wanaume watenganishwe. Kusije tokea munkari utakaosababishwa na migusano; mwishowe tukapata KATIBA MBOVU. Kama mjuavyo kwa wenzangu mliosoma 'magnetics': 'Like poles repel', but 'unlike poles attract'. Kwa hivyo kuwaweka jinsia moja mahali pamoja haitakuwa tatizo; maana watajitahidi ili watengana, kwani siyo dili mwanamume kugusana na mwanamume mwenzako kwa mfano. Lakini mkifanya kinyume, shauri zenu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...