Mwenyekiti wa chama chama cha CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwahutubia Wananchi na Wanachama wakareketwa wa chama hicho,mapema leo jioni kwenye kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho,yaliyofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine,jijini Mbeya,Pichani kulia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishuhudia tukio hilo.
 Sehemu ya Umati wa Watu waliofika kwenye shamrashamra hizo leo.
Mwenyekiti wa chama chama cha CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwa ameshika jembe na nyundo,ikiwa ni alama ya Mkulima na Mfanyakazi mara baada ya kuwasili jioni ya leo kwenye kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho,yaliyofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine,jijini Mbeya,Pichani kulia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishuhudia tukio hilo. 

Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wasanii mahiri wa Filamu hapa nchini,mara baada ya kuwakabidhi kadi za kujiunga na chama cha CCM jioni ya leo.Pichani nyuma kabisa ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana.

Katibu wa NEC, Itikadi,na Uenezi CCM Taifa,Nape Nnauye akiwatambulisha baadhi ya Wasanii nyota wa Filamu hapa nchini,ambao kwa nia thabiti wameamua kujiunga na chama hicho,wakiongozwa na Jacob Steven a.k.a JB,Blandina Chagula,Mboto,Irene Uwoya,Single Mtambalike na wengineo.
Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Kikwete  akimkabidhi zawadi ya gitaa Msanii maarufu wa jijini Mbeya,Petrol Abel a.k.a Awil,anaeshuhudia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Katibu wa Uchumi na Fedha,Bi.Zakia Meghji. 
PICHA ZAIDI  YA TUKIO HILI INGIA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mbeya CHADEMA ziiiii!

    Mbeya CCM oyeeeee!

    CCM!,CCM!,CCM!CCM!,CCM!,CCM!,CCM!

    CCM!,CCM!,CCM!CCM!,CCM!,CCM!,CCM!

    CCM!,CCM!,CCM!CCM!,CCM!,CCM!,CCM!

    X TRILLIONI ZOOOTE!

    ReplyDelete
  2. Mbeya Chadema imefunikwa na CCM, mwanzo mwisho!

    ReplyDelete
  3. Chadema ikifanya Mikutano Mbeya wanao jaza Uwanja ni Oya oya kwa kuwa kwenye Kura ina ambulia namba za viatu!

    Mwisho watu wanashangaa na kujiuliza rundo lote lile mbona nina Kura mbili tu?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...