Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),  Robin Goetzche (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Dola za Kimarekani 64,000, Mwasisi na Mkurugenzi wa Taasisi ya ACE Africa, Joanna Waddington katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya TBL, Dar es Salaam jana. Msaada huo uliotolewa na TBL kwa niaba ya Kampuni ya Sabmiller Afrika ni kwa ajili ya kusaidia kuboresha ufugaji wa mbuzi, kuongeza uzalishaji wa mazao ya vyakula na sekta ya maji katika Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha.Anayeshudia makabidhiano hayo ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindo.

Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindo akielezea mikakati ya TBL ya kusaidia jamii hasa katika sekta ya maji.
Robin akielezea sababu ziliifanya SABMiller/TBL kuisaidia taasisi ya ACE Africa.
 Mwasisi na Mkurugenzi wa Taasisi ya ACE Africa, Joanna Waddington akitoa shukurani kwa SABMiller/TBL kupatiwa msaada huo muhimu kuboresha maisha ya jamii Arumeru. (PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...