Askofu mkuu wa Dayosisi ya Mwanza Ziwa Victoria (DMZV) Andrew Gulle kabla ya kufunua jiwe maalum la Jubilee alikata utepe kuashiria safari ya maadhimisho hayo kuanza rasmi, ambapo kilele chake kitakuwa tarehe 31 Agosti, 2014.  
Jiwe la jubilee.
Kabla ya Uzinduzi wa kanisa la Imani KKKT Mwanza historia ya ujenzi wa kanisa hadi kukamilika ilisomwa naye Bw. Serafin Kimaro. Jumla ya shilingi bilioni moja na milioni 500 zimetumika kukamilisha ujenzi huo uliotumia miaka takribani 13 hadi kukamilika.
Akishuhudiwa na mamia ya waumini na viongozi wa makanisa mbalimbali Kanda ya ziwa na mikoa mingine nchini ukafika wakati sasa wa mgeni rasmi Mkuu wa KKKT Askofu Dr. Alex Geaz Malasusa kukata utepe kuzindua kanisa la KKKT Imani Makongoro Mwanza. 
Sehemu waliyoketi Kamati ya maandalizi ya Jubilee na Ujenzi.
Sherehe za Jubilee ya miaka 25 ya DMZV ziliambatana na harambee ya ujenzi wa Imani Lutheran Schools mradi endelevu unaotarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni mbili za kitanzania hadi utakapokamilika.

Harambee ilifanyika ikiwa na makusudi ya kukusanya zaidi ya shilingi milioni 250 kwaajili ya kuanza ujenzi ambapo kamati ilivuka malengo kwa kukusanya kiasi cha shilingi  milioni 259,280,000/= zikiwemo ahadi, na taslimu ilikuwa kiasi cha shilingi milioni 58,869,000/=.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...