Na Pamela Mollel,Arusha.
Wahitimu katika chuo cha Biashara na Teknohama Arusha (IBICTA) wametakiwa kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kutafuta masoko nje ya nchi kwaajili ya kutangaza bidhaa za Tanzania hali itakayo saidia uchumi wa Taifa kuwa juu
Wito huo ulitolewa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Sila( SILA VOCATION TRUST ARUSHA) Bw. Adam Shayo juzi wakati alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya kwanza chuo cha Biashara na Teknohama Arusha
Alisema kuwa changamoto kubwa iliyopo ni pamoja na bidhaa za Tanzania kutotambulika katika soko la kimataifa huku akidai kuwa asilimia kubwa ya bidhaa zinazozalishwa hapa nchini zinaubora ukilinganisha na nchi zingine
Aidha aliwata wahitimu kutumia stashahada zao katika kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kutafuta masoko nje ya nchi kwaajili ya bidhaa zinazozalishwa hapa Nchini
Kwa upande wake Mkurugenzi wa chuo hicho Bw.Valentune Ndanu alisema kuwa waliohitimu katika chuo hicho ni wanafunzi 10 huku akidai kuwa elimu waliyoipata wahitimu hao itawawezesha kufanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu
Pia alitaja faida nyingine watakayofaidika nayo ni pamoja na kutambua fursa zilizopo sanjari na kujiingiza katika ujasiriamali hali itakayowasaidia kuwa na ajira ya kudumu
Malengo ya chuo hicho ni kutoa digrii ya biashara na teknohama hali itakayosaidia vijana kujiingiza katika ujasiriamali,
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...