Familia ya Ruguyamheto inapenda kutoa shukrani za dhati kwenu nyote kwa misaada na faraja mliyotupatia wakati wa kumwuguza mpendwa wetu Alice,na baada ya kutwaliwa kwake kutoka Dunia hii tarehe 25,Decemba 2013 katika hospitali ya Manipul,Bangalore, India.

Si vyepesi kwetu kuwatambua kila mmoja aliyehusika binafsi, lakini ni vyema kutambua juhudi za Dk Kapiteni wa hospitali ya TMJ na wasaidizi wake: Madaktari na Wauguzi pamoja na madaktari Somshager and Dinesh Kini na wasaidizi wao:Madaktari na Wauguzi ambao walifanya kila jitihada kuokoa maisha ya Alice lakini haikuwezekana.

Tunawashukuru sana marafiki, majirani,jamaa na ndugu wote pamoja na Asasi na Taasisi kwa misaada yao na faraja.

Tafadhari tunaomba mpokee ujumbe huu kama shukrani zetu kwenu nyote!
Ibada ya Shukrani ya kufikisha siku 40 itafanyika siku ya Jumamosi, tarehe 8 Februari katika kanisa la Anglikana la Mt. Mikael, Kunduchi Dar es Salaam , kuanzia saa 3 asubuhi.

“Niliposema, Mguu wangu unateleza; ee Bwana, fadhili zako zilinitegemeza.
Katika wingi wa mawazo ya moyoni mwangu ,Faraja zako zaifurahisha roho yangu.”

Zaburi 94;18 na 19

Mungu awabariki nyote kwa wema wenu, Amen.

Joseph Rugumyamheto, na wanawe , Niyongabo, Jerome na Alexander

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...