Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo (kushoto) akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza Uzinduzi rasmi wa Mashindano ya Safari Lager Nyama Choma 2014,ambapo amesema kuwa lengo kuu la Shindano hilo ni kuongeza hamasa kwa watayarishaji na walaji wa Nyama Choma ili kwa pamoja waweze kufahamu viwango bora katika uchomaji na utayarishaji wa Nyama Choma.Kulia ni Jaji Mkuu wa Mashindano ya Nyama Choma nchini,Lawrence Salva. 
 Jaji Mkuu wa Mashindano ya Nyama Choma nchini,Lawrence Salva (kulia) akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) kwamba katika zoezi hilo la kumsaka mchoma nyama bora hapa nchini,kuwa kutakuwa na vigezo mbali mbali vitakavyotumika kufanikisha zoezi hilo,ambapo alivitaja baadhi ya vigezo hivyo kuwa ni Usafi wa Mazingira,Vifaa vya Kufanyia Kazi,Joto Maalum ya Uchomaji Nyama na vingine vingi. 
 Mratibu wa Shindano la Safaro Lager Nyama Choma,Peter Zacharia (kushoto) akisisitiza jambo wakati akitaja mikoa itakayoshiriki kwenye Shindano hilo,ambayo ni Mbeya,Mwanza,Kilimanjaro na Jiji la Dar es Salaam.Kulia ni Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo
 Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo akikabidhi Kombe kwa Jaji Mkuu wa Mashindano ya Nyama Choma nchini,Lawrence Salva,litakalokabidhiwa kwa Mshindi wa Kwanza wa Safari Lager Nyama Choma.anaeshuhudia katikati ni Mratibu wa Shindano la Safaro Lager Nyama Choma,Peter Zacharia.
Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo (kushoto) pamoja na Jaji Mkuu wa Mashindano ya Nyama Choma nchini,Lawrence Salva wakikata moja ya nyama iliyokidhi viwango vya kuliwa na mlaji wakati wa uzinduzi rasmi wa Mashindano ya Safari Lager Nyama Choma uliofanyika leo jijini Dar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...