Hatimaye bendi kongwe, bendi pekee ambayo imepata kuwa mabingwa wa muziki nchini mara zote mbili ambazo mashindano hayo yamepata kufanyika, bendi ya Mlimani Park Orchestra “Sikinde Ngoma ya Ukae” imeanza kuipua nyimbo zake mpya zitakazokuwa katika album mpya ya “Jinamizi la Talaka” itakayozinduliwa mwaka huu 2014.
Album hiyo itakuwa na jumla ya nyimbo 7,ambapo mpaka sasa Sikinde wameishazitoa nyimbo tatu.
Nyimbo hizo ni Jinamizi la Talaka, Za Mkwezi Mbili,Nikipata Nitalipa.
Nyimbo hizo unaweza kuzisikiliza online au ku-download kwenye mtandao wa https://www.hulkshare.com/sikinde
Nyimbo 4 zilizobakia ambazo nazo zitatolewa muda wowote kuanzia hivi sasa ni 1. Kibogoyo, 2. Dole Gumba, 3. Ng'ombe Haelemewi na Nundu na 4. Tabasamu.
Hii ni album ya kwanza kutolewa tokea mwaka 2009 iliporekodiwa album ya “Supu Umeitia Nazi” album iliyomfanya mwimbaji wake Karama Regesu kuchukua Zawadi ya Tuzo katika Kili Music Award ya mwaka 2009 kwenye category ya “Mtunzi Bora wa Muziki”.
Tunasubiri kwa hamu nyimbo hizi, hatimaye.
ReplyDelete