Hatimaye bendi kongwe, bendi pekee ambayo imepata kuwa mabingwa wa muziki nchini mara zote mbili ambazo mashindano hayo yamepata kufanyika, bendi ya Mlimani Park Orchestra “Sikinde Ngoma ya Ukae” imeanza kuipua nyimbo zake mpya zitakazokuwa katika album mpya ya “Jinamizi la Talaka” itakayozinduliwa mwaka huu 2014. 

Album hiyo itakuwa na jumla ya nyimbo 7,ambapo mpaka sasa Sikinde wameishazitoa nyimbo tatu.

Nyimbo hizo ni Jinamizi la Talaka, Za Mkwezi Mbili,Nikipata Nitalipa. Nyimbo hizo unaweza kuzisikiliza online au ku-download kwenye mtandao wa https://www.hulkshare.com/sikinde Nyimbo 4 zilizobakia ambazo nazo zitatolewa muda wowote kuanzia hivi sasa ni 1. Kibogoyo, 2. Dole Gumba, 3. Ng'ombe Haelemewi na Nundu na 4. Tabasamu.

 Hii ni album ya kwanza kutolewa tokea mwaka 2009 iliporekodiwa album ya “Supu Umeitia Nazi” album iliyomfanya mwimbaji wake Karama Regesu kuchukua Zawadi ya Tuzo katika Kili Music Award ya mwaka 2009 kwenye category ya “Mtunzi Bora wa Muziki”.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Tunasubiri kwa hamu nyimbo hizi, hatimaye.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...