Ujumbe wa Ankal kwa wadau ni kwamba, pamoja na kazi nyingi ikiwemo kubeba boxi lakini hakuna raha kama ya kutumia muda wako wa ziada (kila upatapo nafasi) kuutumia ukiwa na familia yako. Familia ndiyo muhimili muhimu katika maisha yako. 
Ni raha ilioje uonapo mng'ao wa furaha katika jicho la mwanao unapomtoa out kila upatapo nafasi. Kwa umri wake tendo hilo atalikumbuka milele. Na yeye atawafunza wanae na wajukuu faida ya kuwa pamoja kifamilia. 
Fikiria; hizo pesa na muda unavyotupa pembeni (ambavyo ni mara mia ya gharama ya kuitoa familia out) zina faida gani katika maisha yako. Ankal anasema; JALI FAMILIA YAKO hata kama ni kwa mara moja kwa mwezi. Utafurahi nao watafurahi na Mola atakuafu. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. Hahahahahahaha Ankal, umependeza sana. Mungu akubariki wewe na familia yako.
    Mimi,
    andyagne@hotmail.com
    Mdau wako

    ReplyDelete
  2. Hello Ankal,
    Habari.
    Ooh umependeza sana pamoja na familia yako.
    Mungu akubariki
    Mimi,
    Andyagne

    ReplyDelete
  3. Hello Ankal
    Umependeza sana pamoja na famili yako.
    Mungu akubariki

    ReplyDelete
  4. Issa hiyo soda uzushi, pembeni yake kuna kitu cha ngao kaka. Mrudishie motto soda yake. Ha ha ha!!

    ReplyDelete
  5. The mdudu,,du mbavu zangu yaani mjomba umenikumbusha enzi za lodi rofa hilo pama kiujumla nimependa ujumbe wako pamoja na hiyo fekesheni yenu,,tatizo linalowakumba wadau wako mpaka wasahau familia zao ni NYUMBA NDOGO maana nyumba ndogo masharti yake wee acha tu mjomba hawezi kukupa huo muda,,ila kutokana na huo ujumbe wako muuurwa wengi utawatoa kwenye KITANZI,na ujiandae na mvua za COMMENT KUTOKA KWA WADAU WAKO,,na mm the mdudu kuanzia leo naipiga chini nyumba NDOGO ili niwe CLOSE NA FAMILIA YANGU ili niwatoe out kila weekend asante mjomba kwa kunitoa kwenye shimo lenye giza nene.

    ReplyDelete
  6. Ankali,
    Salamakeo wallahi! Yaani katika posti zako zooooote nilizosak oma tokea mwanzo wa libeneke la globu yetu mwaka 2005 hii ni mwisho wa maneno. Yaani umepiga ikulu na wenye kijicho pembe na wanywe sumu wafe! Hakika FAMILIA ndio alpha na Omega ya mambo yote. kwa kweli ankal unastahili nafasi ya kuwa blog nambari One ya kiswahili duniani kote. Huu ujumbe umetugusa wengi. Yaani kuanzia leo I must spare time for quality time with my family!!!!

    ReplyDelete
  7. Anko Umependeza sana sana na familia
    Manshallah ! Mungu akukuzie na kuwapeni Amani na Upendo.
    wadau
    FFU Ughaibuni

    ReplyDelete
  8. MESSAGE SENT ANKAL....BIG UP.....WADAU HUWA TUNAJISAHAU SANA!!!!

    ReplyDelete
  9. Duhhh Mjomba Michuzi ama kweli unajua 'kuyachambua maisha kama karanga'!

    Yaani Ankali ninacho kukubali ni kuwa wewe ni mtaalamu mzuri sana wa kuchagua sehemu za mitoko na mapumziko nafamilia yake tena sehemu nzuuuri kwa bei nafuu.

    Nadhani Mhe. Raisi Kikwete angekupanga kwenye Kamati za Uchumi na Mipango ungefiti sana!

    ReplyDelete
  10. Ankali wewe mtaalamu sana wa 'Kulenga' kama yule Msela aliyeimbwa kwenye wimbo Side Mnyamwezi! ambaye anashinda Masaki wakati kwao kukiwa ni Magomeni!

    Mjomba unajua sana kuchagua sehemu za Starehe bomba kwa nusu bei ama bureee kabisa!

    ReplyDelete
  11. Ankali unajua saaana kulenga sehemu za matembezi na starehe kama Msela aliyeimbwa kwenye muziki 'Side Mnyamwezi' !!!


    Hapo picha ya kwanza na hilo shati lako na kofia la heti ukiangalia bahari ndio tutakupa heshima yako kwa Utaalamu wa kulenga!

    ReplyDelete
  12. Asalam Alaykum, ankala hayo ndiyo maneno, wababa wote igeni mfano huu tosha

    ReplyDelete
  13. Hongera sana ankal. Hakika ushauri wako ni wa busara sana na pia ni wa kumpendeza mola wetu. Watu wengi wasichokijua ni kuwa, pamoja na pesa nyingi, mali nyingi, cheo kikubwa au kufahamika au kuwa maarufu, yote hayo yatakuwa na maana kama familia yako ina furaha na amani. Na hilo huletwa na wewe mwenyewe. Fanyeni uchunguzi, kila mtu kwa wakati wake, hakuna nyumba ndogo iliyowahi kuwa na mwisho mzuri!!!! Mara zote mahusiano ya nyumba ndogo hiushia majuto, simanzi, aibu na fedheha!!!! Iwe mwanamme au mwanamke, nyumba ndogo ni MAJANGA!!! Mungu azidi kukujaalia ankal kwa kuwa karibu na kuipenda familia yako. Mdau, Tabata

    ReplyDelete
  14. uncle hii safi sanaa hongera sana

    ReplyDelete
  15. Tehe teh tee te!

    Misupu bwana.
    Sasa mbona huyo wa kulia mwenye ki blauz cha mistari mistari myekundu, myeupe na mweusi mbona UMEMKATA?

    Tuonyeshe na huyo bhana!
    Huwezi kujua bahati yake labada iko humu humu bulogini kwa Wadau bhana!

    Tehe teh tee!

    ReplyDelete
  16. Nakubaliana na wewe Ankal 101%.Zinazotumika kwenye michepuko ni nying sana.Keep it up Bro

    David V

    ReplyDelete
  17. Ankal umetishaaa naona umeipeleka familia Rudys Farm.....safi sana this weekend na copy na ku paste

    ReplyDelete
  18. naunga mkono hoja 100 kwa 100.nakutakia kila la kheri.wewe mdau hapo juu "salamaleko wallah" ndio manake nini?kuwa na adabu

    ReplyDelete
  19. kama wanavokusifu wewe umependeza, lakini huyo wa pembeni yako kama ni shemeji basi yeye yupo uchi maana hadi matiti yanaonekanwa dunia nzima, kwa mke wa muungwana kuvaa hivo haipendezi kabisa, hasa ukichukulia wewe mbona umevaa nyema sasa kuonesha sehemu za maumbile yao hawa dada zetu ndio urembo kwao. nijuavyo mimi hakuna dini hata moja iliyoruhusu dressing style za kuonesha private parts otherwise wasio na dini na wasioamini kwamba baada ya kufa kutakua na masuali ya kila kitendo ulichokifanya ulipokua duniani. KAMA MUNGU HAYUPO SAWA, JE KAMA YUPO!!!

    ReplyDelete
  20. Ama kweli Mjomba Michuzi wewe ni Profesa mkubwa sana wa Uchumi kwa kubana matmizi huku ukiipa nafasi familia yako!

    Nakumbuka uliweka Posting moja ya sehemu hapa Dar ambapo ni mahala pa matembezi maeneo ya Giraffe Hotel Mbezi Beach pa Kiwango cha matawi ya juu lakini Kiingilio ni Bureeee!

    ReplyDelete
  21. Asante kwa kutukumbusha kwamba pamoja na kukimba kimbia tukitafuta maisha tukumbuke kutenga wakati wa kuwa na familia zetu...Ni ujumbe muafaka unaohitajika wakati huu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...