KAMPUNI ya CXC ya jijini Dar es Salaam, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na waandaaji wa Tamasha la Pasaka wamejitosa kupiga tafu Mkutano Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) utakaofanyika kesho.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando, alisema NSSF imetoa udhamini wa ukumbi wakati CXC na Tamasha la Pasaka kila mmoja ametoa Sh milioni moja kwa ajili ya mkutano huo utakaoenda pamoja na Uchaguzi Mkuu wa chama hicho.
“Tunashukuru Kampuni ya CXC ya jijini Dar es Salaam, waandaaji wa Tamasha la Pasaka kampuni ya Msama Promotions na shirika la NSSF wametusaidia kwa kiasi fulani mkutano wetu.
“Bajeti yetu ni kubwa sana ni zaidi ya Sh milioni 10 maana licha ya wanachama wa Dar es Salaam pia tuna wanachama kutoka mikoani, ambapo wengine wanatoka Morogoro, Tanga, Zanzibar na Arusha,” alisema Mhando na kuongeza kuwa wanatarajia wanachama 150 washiriki mkutano huo.
Alisema mkutano utafanyika ukumbi wa NSSF Waterfront Dar es Salaam na kwamba wanachama kutoka nje ya Dar es Salaam wanatarajia kuwasili leo tayari kwa mkutano huo wa aina yake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...