
Dual Citizenship ni :
1. Kwa Ajili ya Wewe
2. Kwa Ajili ya Nchi
3. Kwa Ajili Ya Watoto Wako
4. Kwa Ajili Ya Maendeleo ya Nchi
The government has said that it is high time now for Tanzania to allow dual citizenships so as to enable the Diasporas contribute to the country’s development in terms of income and expertise.
It has been said that many wealthy and well educated Tanzanians living abroad fail to contribute to national development because they are denied the right to dual citizenship.
The Minister for Foreign Affairs and International Co-operation Bernard Membe said this when he was launching a new outreach project for Tanzanians living abroad prepared by the Tanzanian Diaspora department and International Organisation for Migration (IOM) called on all citizens, politicians and academics to support the inclusion of dual citizenship in the new constitution.
ebu rekebisheni hiyo, "We Tanzanians in the Diaspora ...
ReplyDeleteSio wote tunaotaka uraia pacha, n wachache na waziri wenu.
Mbona nchi zingine mkiambiwa mlipie viza mamilioni mnatoa lakini ubahili kulipia kibali nyumbani kwenu?
Muwekezaji wa ukweli hajali kufuata masharti.
Ni kwa ajili yako - siyo kwa ajili ya wewe
ReplyDeleteThe moment dual citizenship is allowed in Tanzania, then I will apply for the British citizenship immediately.
ReplyDeletehamna hiyo,kama umeamua kuukana uraia sioni sababu ya kuung'ang'ania tena.ama rejesha uraia wa watu urudi kundini.labda lowasa awe rais ktk muungano wa serikali 3.chagua 1
ReplyDeletekama huna uraia wa Tanzania manake si Mtanzania.
ReplyDeleteMany wealthy and well educated tanzanians living abroad...... pooooohhhh
ReplyDeleteHuku wataka na kule wataka....
ReplyDeleteNa hivi tunakuja na national IDs; itabidi mchague moja tu.
I mean for security purpose; mujege tu kutembea kama watalii
Wachangiaji hap wengi roho mbaya tu. Mpende msipende uraia pacha utapita. Kwanza wakubwa wengi wane ndugu Na Jamaa nje. Ni bora kuruhusu ili vitega uchumi virudishwe nyumbani. Utafiti umeonyesha nchi nyingi zenye uaia mbili raia pasha wamefanya maendeleo makubwa nyumbani na hupeleka peas Na utaalaamu nyingi kuchangia maendeleo. Wengi waliochukua uraia nje Si kea sababu ya Kaukauna uraia Ni hail ya uchumi mbaya Tanzania Na uongozi mbaya WA nchi.
ReplyDeleteTAFADHALINI WAHUSIKA HAYA MABO YA URAIA HUKU NA HUKU HAKUNA NA ISITOKEE HATA SIKU MOJA TANZANIA HATUTAKI WALIOBADILISHA URAIA HAWAKULAZIMISHWA WAO WENYEWE WALIKULA KIAPO CHA KUUKANA URAIA SASA INAKUWAJE LEO WNAUTAKA TENA . BINADAMU AU MWANAUME ,MWANAMKE ALIEKAMILILKA HUA ANAUCHAGUZI WA KITU KIMOJA SIO HUKU NA HUKU KAMA MALAYA WA SINZA .
ReplyDeleteHATUTAKI HATUKANI KAMWE KISITOKEE KITU KAMA HICHO NCHI KWETU.
ELIMU GANI MLIOKUWA NAYO NINYI MPAKA TAIFA LIWAHITAJI NYIE NO NO NO NO ! NEVER KWANZA MMEKUWA KINA NANI NINYI PASI YA UK NA PASI YA ADAM NA HAWA? HAHAHAHAHAH! MAJANGA HAYO AU VITUKO, KAMA MMECHOKA BEBA BOX RUDINI KWA MAMA ZENU VIZA INAPATIKANA KIRAHISI SANA NI SIKU 90 KAMA UMEPENDA UNA EXTEND ANOTHER 90 DAYS IKIISHA NA HIYO UNAKITOA LA SIVYO UNA MIGRATION CASE OF OVER STAYING. UKUSHIKWA NI JELA MIEZI MIWILI NA DEPORTATION YA MIAKA 5 BILA KUINGUIA TENA BONGO, HATA KAMA MAMA YAKO ANAFARIKI NDIO SOORRYY TENA-.
MNGEFIKIRIA KABLA YA UAMUZI WENU WA KUUKANA URAIA WA TANZANIA. MMEONA NEEMA INAANZA KUPATIKANA NDIO LEO MNAIOANA BONGO BOMBA?
HATA IWE VIPI WATANZANIA MSIKUBALI KITU HIKI HAKUNA ! WAFANYE UHALIFU TANZANIA WAKIMBILIE UK. NA HUKO WAKIKOROFISHA WAKIMBILIE BONGO ? SWAIN WAKUBWA WATANZANIA MSIKUBALI HATA HII DUNIA IPASUKE-
NI MIMI MTANZANIA MWENYE UCHUNGU NA NCHI NIMEFANYA KAZI ZA KUJENGA TAIFA HILI MPAKA TUMEFIKA HAPA ETI LEO WAO WANATAKA ULAINI KWA SABABU MNAKAA MAREKANI , CHUNIKENI HUKO HUKO.
Nakupongeza kwa ujasiri wako tupo pamoja. Tanzania haihitaji dual citizenship. Wajerumani mpaka leo hawakubali dual citizenship na walijua hasara na faida zake. Hao wamesikia gesi na mafuta wanalazimisha. NO MEANS NO DUAL CITIZENSHIP.
DeleteUwongo mtupu kuhusu Ujerumani.... Wengi wana passport mbili au hata tatu! Wajerumani wanakataa pasi pacha kwa nchi kadhaa... Punguza mbwembwe za uwongo
DeleteMTAJIJU KILICHOWAFANYA KUUKANA URAIA. KUJA BONGO MSISAHAU NI VIZA HILI SIO SHAMBA LA BIBI-
ReplyDeleteBINAFSI KILA NINAYE MJUA ANAISHI NJE HASA ULAYA AU MAREKANI BASI MOMO MWENYEWE NITAKUWA INFORMER WA IMMIGRATION OFFICE KUVUJISHA NANI ANA NYUMBA KINYUME CHA SHERIA NA NANI ANABIASHARA KINYUME CHA YEYE KUWA MTANZANIA HALISI YAANI KAZI MNAYO LABDA BAADA YA 2050
Kuna-wabongo kazi yao ni kuwachana wenzao mbavu" hahaha !!!
ReplyDeleteHata uandike kwa herufi kubwa uraia pacha utapatikana tu. Na tutakula huku na huko wee ulie tu. Huku tutapiga box Na kuendesha Mercedes Benz Hamna shida ya maji wala umeme Na familia zetu tutahakikisha maji na umeme unapatikana kwao.
ReplyDeleteDuh! Yaani kuna wabongo wana chuki si mchezo. Huyo jamaa aliyekomaa na herufi kubwa anaonekana kabisa ana chuki na hasira kwa kuwa anapigika Bongo, sasa akiona wenzie wana uwezo wa kuingia Bongo na kutoka kiulaini, roho inapinda!!
ReplyDeleteAcha chuki na nongwa ndugu yangu, hiyo nchi si yako peke yako, ni yetu sote. Isitoshe, uraia pacha ukiruhusiwa, wabongo wenzio wenye uzoefu wa maisha ya huku nje (ambapo najua pia unakutamani) watakufundisha na wewe ujanja wa kutoka, ili ujielimishe zaidi jinsi watu wanavyoishi hapa duniani.
Na yule mdau mwengine hapo juu anayejifanya kuwa yeye ni mwanadaispora asiteutaka uraia pacha, si kweli. Huyu lazima atakuwa ni wale wale baadhi ya wabongo wenzetu hapo nyumbani, ambao roho zimepinda, na wengi wao hawana maendeleo yeyote ya maana.
Nina imani kabisa watanzania wote waliopo nje wanataka uraia pacha, na wengi walioelimika Bongo, na ambao hawana ugumu wowote wa kwenda nje wakitaka, pia wanaunga mkono suala la uraia pacha.
Bado nasisitiza kwamba uraia pacha ni kwa faida ya nchi na vizazi vyake, na si kama roho pinda wanavyotaka watu waamini.
Asanteni.
It unfortunate but I will be one of the first people not to support dual citizenship.
ReplyDeleteAs per your post and I quote:
"The government has said that it is high time now for Tanzania to allow dual citizenships so as to enable the Diasporas contribute to the country’s development in terms of income and expertise"
Do you mean to say the government does not allow for diaspora to contribute in it's current form of single citizenship? The truth is if the country can welcome foreign investors it does welcome diaspora as well with all the incentives initiated by the law and rule.
To me its a shallow point to justify dual citizenship. If a diaspora want to share his expartise and knowledge which he acquired through Tanzanian Tax payers money he can do it and that is patriotism and not selfishness or selfish motives as propagated by diaspora.
Second point qoute:
."It has been said that many wealthy and well educated Tanzanians living abroad fail to contribute to national development because they are denied the right to dual citizenship".
Can any diaspora mention one wealthy and well educated Tanzanian diaspora who has been denied that right? For the development of his kin and kith? What contribution has any diaspora done for the nation maybe for their personal enrichment without regards to the development of the country or it's genuine people who don't have the ability to have another citizenship. Another shallow reason for allowing dual citizenship.
Jamani Watanzania wenzangu,
ReplyDeleteSuala hili ni muhimu sana ial tuangalie vizuri tusikurupuke tu na kusema uraia pacha. Hii kitu lazima iandikwe au iwekwe vizuri na si kila mtu mtu aje kuomba uraia wa Tanzania.
Kwenye swala la ulinzi ni muhimu na fasaha kwa serikali kuchukua tahadhari kwani huwezi jua unatoa uraia tunakuja kuongozwa na mgeni toka nje (mkoloni kurudi mlango wa nyuma). Hata nchi zilizokubali uraia pacha kama Kenya hawajaweka kuwa ndio kila mtu aje kuomba uraia na kuwa uraia pacha. Wameweka udhibiti wa hali ya juu na hao jamaa ni kuja kutembea tu kwa hata uongozi hawawezi kugombea.
Halafu si lazima kuwa tuwe na uraia pacha, bali tunaweza kuweka mazingira fulani kuwaruhusu watanzania wazawa tu kuwa hata kama umechukua uraia wa nchi nyingine wewe bado unaweza kuja Tanzania na kuwekeza au bila viza. Kitu kama ukazi wa kudumu(permanent resident)ambacho hata wachina/ wamarekani wanakitumia. Uraia pacha sio lazima, cha msingi ni kupigania haki ya uzawa kutokufutika.
Kuna mijitu inafikiri unapozungumzia 'kujenga nchi' ni lazima uwe unaishi bongo, mchango wetu diaspora kwenye uchumi ni mkubwa sana japokua hatuishi nyumbani. Watu tunatuingiza hela kila mwezi kwenye circulation, watu tuna mabiashara huko na tunatoa ajira wakati kuna wachangiaji hapa mlioko bongo ambao hata kazi hamna, hamlipi hata kodi, yani mna zero contribution kwenye uchumi wa nchi.
ReplyDeleteBut I thought US law didn't permit one to be a dual citizen, that if you were (by birth or otherwise), you either had to give up the other citizenship when you came of age, or else you'd lose your US status. And that if you became a citizen of another country, you'd automatically lose your US citizenship. So what's all this talk about dual citizenship?
ReplyDeleteHmmm, is the USA the only other country in this world?... How about me, half Egyptian?
DeleteYour wrong,in USA we allow dual citizenship.
DeleteI am a Tanzanian and American Citizen. I personally don't like the Idea of Dual Citizenship because it doesn't make any sense.
ReplyDeleteI love my motherland Tanzania only because of its beauty. The Kilimanjaro the tallest of all in Africa, Lake Victoria the biggest of all in Africa, Lake Tanganyika the deepest of all in Africa, Zanzibar Unguja and Pemba. Fertile Land, Natural Resources and other attractions Forestly and National Parks. I love the Food of Tanzania, Pilau, Chapati, Uji, Kachumbali and Mtori.
As an American Citizen and Tanzanian by Birth, I will contribute to the Tanzania economy ONLY by way of TOURISM. Vist the KILIMANJARO, ZANZIBAR, PEMBA , UNGUJA, MIKUMI, VICTORIA ,TANGANYIKA, SERENGETI, NGORONGORO AND MANY MANY MANY OTHER SITES.
My Fellow Diaspora, if you really in LOVE with Tanzania and you want her to PROSPER, TOURISM is ONLY WAY out to Boost her Economy.And that does not necessary need to have Dual Citizenship.
If you work, Live or own a business abroad say; Australia, Britain, Brazil, China, USA or India, you will be able to spend 10,000 or More USD in Tourist alone. And that is lots of money in contributions to the ECONOMY.
Another way out is Philanthropic
Visiting Schools, Hospital and other Charitable Organizations in Tanzania. You don't have to give money to these Institutions but, you can Volunteer for a Week or two. You can also TEACH classes for two weeks of your vacations as PUBLIC SPEAKER Say MOTIVATIONAL SPEAKER.
All these I mentioned above does not require "DUAL CITIZENSHIP"
Speaking ONLY as US citizen.
By LAW: Your required to file Taxes each YEAR for all income generated outside the United States and the Internal Revenue Authority will take more that 30% of your income. So, be informed when doing business in two territories.
Let say your business became successful in Tanzania. The Tanzania Revenue Authority they want more that 25% of your income and IRS also will require 30-40% of your income. If you evade these Taxes the American GOV will go after your asset in Tanzania.
So, my advice just stay in one Territory and you will live a happier LIFE.
Alexander Fumbuka- Founder
Alexander Global Furniture
8521 Long Point Road
Houston, TX 77055
Safina USA
Charitable School & Medical Supplies
Houston, TX.
Yep! It is best you stay a tourist in TZ... One thing is sure, when dual citizenship passes, you will be the first one in line to demand you right retire in Tz.
DeleteI think your problem is that you had such bad experiences in Tanzania that you do not want to return, as for the rest of us, we love our home and look for every opportunity to come back home and establish ourselves here...Perhaps reselling furniture is difficult in TZ in view of the stiff competition but making a toothpick factory here from your furniture could work!! Karibu nyumbani mzee, hatuta kusahau, ukipachoka majuu, tutakupokea nyumbani!
Urais wa Tanzania si mali chochote. Kwa wasiosafiri ni kitu muhimu sana. Kwa wenye kutaka kusafiri na kuishi sehemu yoyote duniani uraia wa bongo ni sawa na takataka yoyote.
ReplyDeleteTatizo la wanaotetea uzalendo ni ufisadi. Mnataka tuwekeze huko wakati hamtaki kutusikiliza. Endeleeni kulana kama samaki geuzaneni asusa mtakavyo. Inakuwaje magabacholi wana uraia wa zaidi ya nchi moja na mnawakubali lakini waswahili mnawatilia mtima nyongo kama siyo roho mbaya tu?
Sasa kama hakuna shida ya umeme sijuhi maendesha Benz...si mutuwache na umasiki wetu????
ReplyDeleteKwanza mnajisumbua...hakuna ajenda ya uraia wa nchi mbili hivyo hata Bunge la katiba haliwezi kuwa discuss kwa kuwa hawana authority ya kuongeza agenda zao...Warioba alishamaliza kazi yake....
Watu tumesoma nje nchi mbali mbali...lakini kwa uzalendo na nchi zetu hatujawahi kufikiria kukimbia ...tumekuwa loyal na kurudi kulitumikia Taifa....
Nyie endeleeni kuwatumikia wazungu...hamkatazwi...
Hakuna uhusiano kati ya remittance na uraia wa nchi mbili...kama utataka kuwasaidia nduguzo utatuma tu ela hata kama wewe mmarekani...
Kama hujawahi tuma chochote kwenu hata uwe na uraia wa nchi TATU utabaki hivo hivo...kutumikia tumbo
Kwanza nashangaa wa Tz gani wanakana uraia...niliposoma kote wa Tz tunasifa ya kurudi nyumbani baada ya kumaliza masomo...
Jaribu kufanya kazi Siemens defence research au BAE na pasi ya kitanzania? Hata kazi ya kusafisha sakafu hutapata.. Tupo wazalendo ambao tumefanya kazi kuijenga Eurofigher Typhoon, experience hiyo tusingeweza kuipata tungeng'ang'ania pasi ya kibongo... Kuna maeneo mengi tu wazalendo wameweza kufanya kazi ambapo kazi isingepatikana na,pasi ya kibongo
DeleteWadau punguzeni hasira na mjadili suala hili kwa kina, subira na staha. Hili si jambo la kishabiki bali ni jambo lenye National interests ,hivyo hakuna haja ya majibizano ya aina hiyo hapo juu kwani mwisho wa siku ni sheria ndio itafuatwa,sasa kama sheria itasema ndio kwa uraia pacha ni sawa na ikisema hapana pia ni sawa hakuna haja ya kubezana hapa bila msingi. .changia hoja yako kwa misingi au hoja zenye msingi..ndio demokrasia inavyo tufundisha na si Vinginevyo. .
ReplyDeleteMnaopinga uraia pacha ni malimbukeni tu. Hao maponjoro mnaowapa uraia wa Tanzania kila kukicha wakati wana uraia wa India, UK, na Canada muwanyanganye urai kwanza kabla ya kuwakatalia wazawa kupata urai pacha!! Nyambafu!!
ReplyDeletePlease sign the petition more votes zinahitajika.
ReplyDeletetumetofautiana sana kimitizamo, nahisi itatuchukua kipindi kirefu sana kugundua wenzetu walipo.. wachilia mbali kuwafikia
ReplyDeletehivi kama kuna mzawa ameukana uraia wa Tz halafu tena kila unadai kuutaka uraia wa TZ kweli ana akili nzuri? wewe mwenyewe umeukana uraia wa TZ ukiwa na akili timamu halafu kila ukimuona JK na Membe unakazi ya kuwaomba uraia wa nchi mbili hivi akili zako zinakutosha kweli? unaona matapishi yana thamani kwako unataka kuyalamba tena? hebu kaeni na uraia wenu huo mnao uona bora huku kama mnataka mje kuwekeza kama wazungu wanavyofanya mmesikia kuna gesi na mafuta mmeanza kubana pua ooooooh! tunataka dual citizenship. Kaeni na huo uraia wenu mnataka kotekote waone kwanza. Hii ajenda isichukuliwe kirahisi rahisi inahitaji kabisa waTZ wapige kura ya maoni tukiruhusu tu ipo siku nchi hii itakuja kutawaliwa na kina KAGAME maana anaitamani sana Tz.
ReplyDeleteHistoria ya taifa letu ingekuwaje iwapo Mwalimu Nyerere angeamua kuchukua uraia wa Uingereza wakati alipokuwa masomoni, tulijadili suala hili kwa umakini Watanzania.
ReplyDeleteUkweli ni kwamba, Mtanzania anaweza kuishi, kufanya kazi, kumiliki mali, kufungua biashara, na kuwekeza kihalali ughaibuni bila kubadilisha uraia. Kwa yule aliyebadilisha uraia, pale atakapoamua kurudi anaweza kuomba tena uraia wa Tanzania.
Kupata uraia wa nchi ya kigeni kuna faida zake nyingi sana, wingi wa faida hizo usitufanye tufumbie macho changamoto zake. Wakati sisi tunamezea mate uraia wa nchi za wenzetu, kuna wale ambao wangeupenda uraia wa nchi yetu.
Kwa njia ya mfano mdogo, kuna raia wengi sana sana wa kigeni walioajiriwa, wanaofanya biashara, na waliowekeza Tanzania ambao kinachowazuia kuchukua uraia wa Tanzania ni kutotaka kupoteza uraia wa nchi walizotoka. Iwapo uraia wa nchi mbili utaruhusiwa, kutakuwa na miminiko mkubwa wa raia wa nje ambao watachukua fursa zaidi za kazi, biashara, na uwekezaki zilizopo Tanzania. Fursa zilizopo Tanzania kwa Mtanzania aliye nyumbani na yule aliye ughaibuni zitapungua kwa kasi.
Kwa heshima kubwa, naomba tulijadili swala hili kitaifa na kwa kina.
Hicho cha kuwapa wageni uraia wa Bongo bila kuhoji uraia wa nchi zao nyingine, na wakati huo huo tunawawekea uzibe wabongo wenzetu, ndio kitu kinachinisikitisha sana. Ndio maana wabongo tunaendelea kuibiwa rasilimali zetu, kwasababu wengi wetu ni wagumu sana kuelewa mambo yanavyokwenda. Chuki na roho mbaya tumeweka mbele!
ReplyDeleteUKWELI NI KWAMBA SIONI HAJA YA KULUMBANA HAPA KWANI URAIA NI HAKI YA MWANAADAMU YEYOTE, HATA WALIOKO NJE AU NDANI YA NCHI HUSIKA SIO KILA MTU NI RAIA HALALI, KWANI WALIPO KUSANYA WAHAMIAJI HARAMI NI SHERIA GANI ILIOTUMIKA??? EBU FUNGUA YOU TUBE ANAGLIA OPERETION KIMBUNGA UENDELEE HADI UPANDE WA RWANDA NDIO UTAJUWA KUWA UTAWALA WA TANZANIA NI WAKICHOYO NA UBINAFSI. WALIFUKUZWA WATU AMBAO WANAHAKI YA KUITWA WATANZANIA KWA SABABU TU WALIKUWA NA MALI NA HUYO KIONGOZI WA OPERATION ALITAMANI VITU VYA WATU HAO. WALIPO HOJIWA HUKO RWANDA WALIKUWA HAWAJAWAHI KUKANYAGA NDANI YA NCHI HIYO TANGIA KUZALIWA SASA JEEE UMEMFUKUZA MNYARWANDA ALIE ZALIWA NDANI YA TZ NA HAKUWAHI KUUKANA U TZ NA SASA ANAWAJUKUU JEE HAKI IKO WAPI HAPA, NANI MTZ NA NANI SIE???? NAISHIA HAPA MIMI SINA LA ZIADA ISIPOKUWA TUANGALIE SAAANA KWANI HII DUNIA HAINA MWENYEWE. (NB:HIZO YOUTUBE ZIKO NYINGI KAMA UNAOMDA WA KUTOSHA USICHOKE KUPEKUWA UTAYAONA MENGI YA ROHO MBAYA ZA NDUGU ZETU WA TZ)
ReplyDeleteNO DUAL CITIZENSHIP, NO!
ReplyDeleteMDAU WASHINGTON, KWANINI LEO WEWE HUKUJUA MADHARA YAKE? TUPIGE HAPA HAPA BOX LINATOSHA TUWAACHE NDUGU ZETU WAJENGE TANZANIA SIO KILA KUKICHA TUWAPE MISUKOSUKO
MLIAMBIWA KAANE BONGO KUJENGA NCHI , MARA OOO HH MBU, MAJI, UMEME, SASA HUKO KIMENUKA HAKUNA MPANGO LEO NDIYO TANZANIA MNAITAMANI
Kwa upande wangu mimi sidhani kama tatizo ni kuwa raia mara mbili bali watanzania wanataka uhuru wao wa kuingia na kutoka katika nchi yao kwa kuwa wamezaliwa humo, swala la kupangiwa mda wa kukaa nchi uliozaliwa halileti udugu wa uzalendo. kuna mchangiaji kasema eti watu watafanya uhalifu na kukimbilia nje, nadhani sio kweli kwani wanaoshikwa na madawa wengi wao wanatoka huko huko TZ, jee kwani uhalifu ni wa mwana Diaspora tuuuuu??? Naomba tujiulize hapo. Mimi niliishi nje kwa mda mrefu nilifanya kaz za serikali nilizaa huko lakini mwisho wa siku niliamua kurudi na sasa ni mwaka wa saba tangia niiache Europe na kwingineko lakini sioni ubaya wa wana Diaspora kuachiwa milango wazi kuingia na kutoka katika nchi waliozaliwa, kwani hakuna mtu yeyote duniani anaeweza kubadili damu ya mtu na kuifanya kuwa tofauti na damu tyake asilia. Ningeshauri wachangiaji na serikali kwa ujumla kuwa watanzania waishio nje wasibughudhiwe wanapo kuja kutuona na wasikadiriwe mda kwani nchi ni yetu sooote. Mr Kutikavu.
ReplyDeleteMa diaspora muendelee kutumia fedha zenu nyumbani, hata unapotuma kwa ndugu hizi pesa zinazunguka kwenye mzunguko wa fedha na kuchangia kujenga uchumi, muwe wawekezaji. Ukweli ni kwamba wakati mwingine credit facilities za nyumbani si rahisi kupatikana kama nje tumieni fursa hizo muwekeze kwenu mtoe huduma mtengeneze faida na ajira kwa wabongo. Tunawahitaji.
ReplyDeleteUraia wa nchi mbili sio wa kukubaliana nao kabisa. Kama umeikana nchi yako ya kuzaliwa, leo unadai tuingie kwenye hili jambo ni kutaka kuleta matatizo makubwa.
ReplyDeleteHata kama kuna watanzania wenye pesa na wamechukua uraia wa nchi nyingine kwanini wasije na miradi yenye tija kwa manufaa ya taifa lote? Hivi kweli mnashindwa kuungana pamoja na kusema hospitali zetu kupata vifaa na vitanda vya kutosha kila mnapo kuja? Yani ubinafsi ndio mwingi sana na hili swala siliungi mkono kabisa kwani hakuna uzalendo hapo hata kidogo.
Najua Tanzania kunamatatizo mengi ambayo kwa akili za kawaida unashindwa kuelewa inakuaje hawa watawala wanashindwa kutatua hizi kero.
Kuna kitu kipo nyuma ya hili swala na hasa watawala wachache. Hivi tunapata mbunge/waziri/raisi ni mtanzania pia ni mmarekani inakuaje kama amekula pesa zetu? Tutamshitaki wapi au hayo hatuyaoni? Au anasepa na tembo wote, hatari sana.
Sisi tuwape watanazania wa kuzaliwa na watoto wao uraia wa Tz.Lakini wageni wasiowazawa wa Tz tusiwape. Basi
ReplyDeleteNIMEANGALIA MAWAZO MENGI YA WACHANGIAJI NIMEONA HIVI:
ReplyDelete1.URAIA PACHA UNA FAIDA NA HASARA ZAKE.
2.WANAOTAKA URAIA WA PACHA WAPATIWE LAKINI WABANWE KUPATA KILA KITU HAPA TANZANIA MFANO SUALA LA UONGOZI WA JUU KUANZIA MKUU WA WILAYA, MKUU WA MKOA NA KWENDA JUU WASIPATE (Mtaruhusiwa kuwa WAJUMBE WA NYUMBA 10 AMA MASHINA YA KATA KIUONGOZI) KWA KUWA HATUWEZI KUWAAMINI SANA tukumbuke suala la PINOHCETI NA FUJIMORI kule Marekani Kusini na Asia kusini mwa Bahari ya Pasifiki).
3.HASARA YA URAIA PACHA
-WENGINE WATAWEZA KUHUJUMU KWA KUKWEPA KODI.
-WENGINE WANAWEZA HATA KUIHUJUMU NCHI NA KUHATARISHA USALAMA WA NCHI.
4.FAIDA ZAKE URAIA PACHA
-WANA DIASPORA KUSHIRIKI KTK UJENZI WA NCHI YAO YA ASILI.
-FAIDA YA UWEKEZAJI.
-FAIDA YA KUHAMISHA TEKINOLOJIA KUJA NCHINI KWA WAFANYAKAZI NA WATAALAMU.
HIVYO TUKUBALI URAIA PACHA LAKINI TUPEMBUE YATAKAYO FAA NA YASIYO FAA KTK HAPO MANNE (4) JUU HIVYO TUPANGE KWA KUKUBALI NA KUDHIBITI HAPO MAJANGA NA KUCHUKUA TAHADHARI NA KUCHUKUA NAFASI YA FAIDA ZILIZOPO.
URAIA PACHA NI MUHIMU TUSIDANGANYANE
ReplyDeleteTWENDENI NA WAKATI http://www.raiamwema.co.tz/uraia-pacha-ni-muhimu-tusidanganyike
Mimi nimeukana uraia wangu na sina haja ya pasi ya Tanzania. Itanisaidia nini? kaeni na umasikini wenu, mimi nitakuja kutembelea jamaa tu. Msijiringie na uraia wenu wakati bado ni ombaomba baada ya miaka 50 ya uhuru. Mnavyoringa na uraia wenu utasema kuwa Tanzania ni Switserland wakati ni moja ya nchi kumi masikini duniani. You can go to hell.
ReplyDeleteUraia wa nchi mbili ni khaki ya kila mzawa, na mwenye asili ya Tz, mradi sheria ipitishwe, sasa nyie ndio nini kuwakataaa, ndugu zenu walioko nje, au ndio wivu na roho mbaya, mwaya, twatumiwa hela na mahitaji yetu toka huko huko nje kwa ndugu zetu walioenda kutafuta na kujali nyumbani, wengine hapa hawana ndugu wa kuwatumia hela toka nje basi wamekalia hatutaki hatutaki, wewe, wengine tunataka kwa ajili ya michango inayochangishwa na ndugu zetu kuletwa huku home
ReplyDeleteSamahani wadau narudia maoni yangu toka habari nyingine kuhusu uraia pacha. Wenzetu Wamarekani wanaangalia je mtu(au taifa) fulani ana faida ghani kwao?(wanaita interest). Wantanzania inabidi waangalie je Watanzania waliopo Ughaibuni wanafaida ghani kwa TZ?! Na nadhani wamefanya utafiti nakuona kweli wana faida. Jamaa wengi wanaongea na kutoa mifano ya ajabu ajabu na si ywa kweli. Mfano, Marekani hawakulazimishi ukane uraia wako ili uwe na wa kwao, bali ukiwa na uraia wao kuna faida nyingi, kama mikopo ya shule, kuingia nchi nyingi bila visa n.k Jamaa wengine hapa wanaingiza jina la Nyerere, kwamba kwa vile alisoma UK angechagua kuwa raia huko.PUMBA! Nakumbuka wakati Nyerere anasema kuwe na vyama vingi watu walipinga sana, kama hivi wanavyopinga huu uraia pacha. baadaye ilibidi tukubali kwani mabadiliko yalikuwa ni lazima(mataifa ya wakubwa yakisema yamesema).Halafu we jamaa uliyesema ilo Unajua kwamba wajukuu wa Kambarage wanasoma na kukaa Marekani?! Unajua viongozi wengi(siyo wachache) watoto au wamesoma au wanasoma majuu?!Halafu sio kila MTZ amekana uraia wake kwa kuchukua uraia mwingine. Mfano mie, wazazi wangu walikuwa tayari wa taifa lingine,lakini nilizariwa TZ. lakini nilipofika miaka 16 nikapewa pass ya nchi nyingine. Nilipoomba pass ya TZ nilizungushwa mpaka leo sijaipata(kwa vile labda siyo mtoto wa fulani). Miaka karibu 20, kila mwaka nakuja Bongo kumwoona bibi yangu, ndugu, jamaa na marafiki. Nimepeleka umeme na maji kwa bibi yangu kwa hela zangu, nasaidia kufundish shule, kuwaletea vifaa kama computers n.k Naleta wageni, tena kundi kama 20-50 wanakuja kutalii na kusaidia shule. Vile vile nina timu(mimi si Kajumulo)kwa hiyo inabidi nitume pesa kila mala. Je watu kama mimi tuna faida ghani TZ? Mie uraia pacha upite usipite ni sawa tu(hamna faida nayopata au kusema natengeneza hela kwa sababu ya gesi au vivutio vingine, lakini nasapoti. Naomba wengine waache kuongea madudu, fanya utafiti kabla ujaropoka. Ndiyo maana ya kwenda shule. Serikali, imefanya utafiti wa kufafanisha mataifa yaliyo masikini kama, Kenya, Nigeria, n.k nakuona faida wanayopata toka kwa jamaa zao Ughaibuni. Nakubalina na mdau aliyesema, kweli Ughaibuni siyo Marekani na Ulaya pekee. TZ inabidi tuwe mstali wa mbele siyo nyuma kila wakati. Mabadiliko yamekuja, upende usipende yatakubadilisha tu.
ReplyDeleteAnayesema hataki uraia kwa sababu ya Tanzania maskini, ukae kimya usiseme namna hiyo maana Mungu anaweza kukugeuzia kibao na ukajutia. Huwezi kumkana Muumba wa nchi yako na aliyekuumba wewe. Kubwa ni maelewano na ushauri ukisema nchi maskini sijui nini, kwa nini usijitahidi kuifanya iwe tajiri? hata ulikokimbilia ulikuta ni matajiri tangu zamani wala si shauri yako. Mtaishi utumwani kama hamna kwenu vile. Ni sawa na kumkana baba au mama yako eti kwa sababu ni chongo au hana mguu. Ni ushauri tu ila marumbano hayafai sie wengine tupo USA, ila tumeridhika na tanzania hiyo maskini, siwezi kumkana mzazi wangu aliyenizaa hata kama ni mbaya kiasi gani.
ReplyDeleteTansanian Diaspora come back home and make a difference: YES WE CAN
ReplyDeletehttp://edition.cnn.com/2014/02/18/tech/winds-of-change-massive-uyi-stewart/index.html?hpt=iaf_t2
URAIA WA NCHI MBILI MWISHO WAKE WATAKUJA MASHOGA KUTUTAWALA.
ReplyDeleteTanzania haitaji urai PACHA. Muhimu ni kuangalia jinsi ya kuwasaidia raia ambao wanajilipua kwenye nchi za wenzetu na kupoteza hadhi ya uraia wa Tanzania. Lakini pia sheria ya kuwasaidia hao isiwape nafasi wale ambao wamejifanya wakimbizi wa Burundi, Somalia, nk. Kisha wakafanikiwa kupata uraia wa nchi nyingine. Muhimu ni kwamba mtu akipata uraia wa nchi nyingine kwanza apoteze uraia wa Tanzania. Akitaka kunufaika na sheria itakayokuwa imetungwa, aombe na aambatanishe passport yake ya nchi aliyochukua uraia. Najua utaratibu wa nchi nyingi, hata uchukue uraia, lakini kwenye passport yako kunaandikwa pia jina la nchi yako ya asili. Hapo anaweza kupewe kadi tu ya kumtambulisha kuwa aliwahi kuwa na uraia wa Tanzania, na hivyo kufaidika na sheria itakayotungwa. Mfano kutembea Tanzania bila ya kuwa na VISA, kuwekeza kwa mashariti nafuu, nk. Lakini uraia wa NCHI MBILI USIRUHUSIWE
ReplyDeleteKAMA NIA YA WABONGO WALIO KWENYE DIASPORA NI KUICHANGIA NA KUINDELEZA NCHI YENU YA ASILI BASI MNAWEZA KUFANYA HIVYO NA MNAKARIBISHWA, NA SIYO KULAZIMISHA KUWEPO KWA DUAL CITIZENSHIP, KWA HIVI SASA BADO NCHI HAIPO INTERESTED KWA HILO LABDA BAADAE ITABIDI KUSUBIRI KWANI UKIANGALIA KWA HIVI SASA NCHI INA NEEMA WAWEKEZAJI WENGI TU AMBAO HAWANA HATA ASILI YA TZ WANAKUJA BILA KUITWA NA WANATOA MCHANGO MZURI, YANI KIFUPI MCHANGO WENU TUNAUSHUKU LKN HATUUHITAJI KIVIIILE KAMA VILE MNAVYOFIKIRIA
ReplyDeleteKweli kazi hipo, jamaa mmoja hapo juu kasema ni PUMBA kutoa wazo kwamba mbona mwalimu Nyerere hakukana uraia wa TZ.
ReplyDeleteHapa tukijiloga tu kuwa na uraia wa nchi mbili, piga hua viongozi wote TZ hii familia zao ndio wataongoza kuwa na uraia wa nchi mbili wakati raia walio wengi maskini watabakia hapahapa TZ.
Hivi wewe mmarekani au mjapani uliyekana uraia wa TZ likija dili la kuuza nchi hii nakupewa pesa utajiuliza mara mbili? Embu tuache utani jamani, viongozi wangapi hapa kipindi hichi wameishi huko ulaya na marekani, wamerudi na kupewa vitengo lakini tunaona hawana uzalendo kabisa, hivyo tusidanganyane.
Watanzania tunakazi sana ya kubadilisha huu mfumo tulio nao kuwa wa haki na utu kwa kila mmoja. Ubinafsi tulio nao ndiyo unatumaliza.
Hakuna uraia wa nchi pacha hapa.
Anonymous wa #50 February 19, 2014. Je umesoma hayo maoni niliyosema kuhusu Nyerere? We unasema "Hapa tukijiloga tu kuwa na uraia wa nchi mbili, piga hua viongozi wote TZ hii familia zao ndio wataongoza kuwa na uraia wa nchi mbili wakati raia walio wengi maskini watabakia hapahapa TZ" Je umesoma niliposema unajua familia za au Viongozi wengi(ukichanganya familia ya Nyerere wanasoma Ughaibuni? Nyerere mwenyewe alisoma Ughaibuni).Unasema familia zao ndiyo watakuwa viongozi, angalia sasa falimia ghani zinongoza TZ!? Kwanza ngoja niache kubishana na wewe, wenye nchi wameshahamua liwe na litakuwa. Na wanaosema jamaa wa Ughaibuni watauzaa nchi, sijui uwe mtu wa namna ghani kutojua hiyo nchi ilishauzwa zamani. Gesi, madini, wanyama kila siku tunaona vinakwenda nje'.
ReplyDeleteTatizo la wabongo wengi wakisikia watu wanataka uraia wa nchi mbili mawazo yao kuwa bongo kuna neema kuliko tulipo kuwepo, lakini wanasahau kwamba sio walioenda tu ndio wanahitaji lakini kuna watoto wao ambao wamezaliwa nje lakini wazazi ni watanzania ni ngumu nimuweke mtoto wangu kwenye passiport ya kibongo awe tofauti na wenzake shuleni. Huko UK shule kila siku wanafanya trip za kishule tunaenda America KWA SCHOOL TRIP mtoto wangu aanze kuomba visa for what nibora awe na Uk tu.
ReplyDeleteMDAU WA 39 ULIYEKANA URAIA WA TANZANIA:
ReplyDelete..............Mimi nimeukana uraia wangu na sina haja ya pasi ya Tanzania. Itanisaidia nini? kaeni na umasikini wenu, mimi nitakuja kutembelea jamaa tu. Msijiringie na uraia wenu wakati bado ni ombaomba baada ya miaka 50 ya uhuru. Mnavyoringa na uraia wenu utasema kuwa Tanzania ni Switserland wakati ni moja ya nchi kumi masikini duniani. You can go to hell....
WEWE NI BWEGE MTOZENI NA TUTUSA LA MWAKA KWA KUKANA URAIA WA TANZANIA WAKATI UKIJUA UNAO NDUGU ZAKO NCHINI TANZANIA UKITAKIWA KUJA KUTEMBEA NA SASA UTAKUJA KWA VISA KWA UBWEGE WAKO!
HERI UNGESUBIRI URAIA PACHA ILI UPATE KOTE KOTE MATROKEO YAKE UMEKUWA MTUMWA UGENINI HUKU UKIUMEZEA MATE UTANZANIA WAKATI UMESHA POTEZA!
MANENO YAKO HAY6O HAPO JUU NI ''SIZITAKI MBICHI HIZI'' !
MDAU WA 39 ULIYEKANA URAIA WA TANZANIA:
ReplyDelete..............Mimi nimeukana uraia wangu na sina haja ya pasi ya Tanzania. Itanisaidia nini? kaeni na umasikini wenu, mimi nitakuja kutembelea jamaa tu. Msijiringie na uraia wenu wakati bado ni ombaomba baada ya miaka 50 ya uhuru. Mnavyoringa na uraia wenu utasema kuwa Tanzania ni Switserland wakati ni moja ya nchi kumi masikini duniani. You can go to hell....
WEWE NI BWEGE MTOZENI NA TUTUSA LA MWAKA KWA KUKANA URAIA WA TANZANIA WAKATI UKIJUA UNAO NDUGU ZAKO NCHINI TANZANIA UKITAKIWA KUJA KUTEMBEA NA SASA UTAKUJA KWA VISA KWA UBWEGE WAKO!
HERI UNGESUBIRI URAIA PACHA ILI UPATE KOTE KOTE MATROKEO YAKE UMEKUWA MTUMWA UGENINI HUKU UKIUMEZEA MATE UTANZANIA WAKATI UMESHA POTEZA!
MANENO YAKO HAY6O HAPO JUU NI ''SIZITAKI MBICHI HIZI'' !
Kazi kwenu ndugu zetu Madiaspora kusuka ama kunyoa!
ReplyDeleteMsimamo wa Tanzania na Chama cha Mapinduzi ni kuwa tunataka kurudisha Azimio la Arusha na baadhi ya vigezo vya Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea,,,hivyo Uraia Pacha hapana!!!
Madiaspora,
ReplyDeleteMkitaka tena Uraia wa Tanzania Mashariti ni haya MANNE hapa chini:
1.MUUKANE URAIA WENU WA MAJUU,
2.MUINGIE UANACHAMA WA CCM,
3.MPEWE KADI ZA KUPIGIA KURA, 4.MPEWE VITAMBULISHO VYA TAIFA,
Karibuni tena na karibuni sana nyumbani Tanzania!
NA NDIO MJE TUWAPE TENA URAIA WA TANZANIA KWA KUWA TANZANIA KAMWE HAIWEZI KUWA NA URAIA PACHA!
Nyie wote mnaowaandamaa Madiaspora, naona mnachuki binafsi kwa sababu wao walifanikiwa kutoka wakati nyie mnapiga maneno hapa. Au wamewachukulia wake na waume zenu, jikazeni tu, kwani kila mtu na bahati yake. Na msilalie bahati ya wenzenu milango wazi, shauri yenu mtaliwaa na fisi. Na wakubwa wameshasema wanataka uraia pacha, kwa sababu watoto wao wengi wako huko na wenyewe wanashinda huko.Poleni sana waTZ msioelewa, lakini mnaandindika humu kama nyie ndiyo mnatoa uamuzi. Nyie wenyewe mliwapigia kura, sana CCM, mtawapinga vipi!? Jamani kubalini matokeo tu, na matokeo yatakuwa mazuri kwenu ingawa hamuoni.
ReplyDelete