Mwenyekiti wa Muda wa Bunge la Katiba,Mh. Pandu Kificho akisisitiza jambo wakati wa Kikao cha Bunge hilo,kinachoendelea leo kwenye Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma.
Wajumbe wa Bunge la Katiba,Mh. Tundu Lissu na Mh. Jussa wakibadilishana mawazo wakati wa kikao cha Bunge la Katiba kinachoendelea leo Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba,Mh. Edward Lowassa akifatilia kwa makini mjadala wa Bunge hilo,mjini Dodoma leo.
Mh. Anne Makinda akichangia Mapendekezo ya Rasimu ya Kanuni zitakazotumiwa na Bunge Maalum la Katiba.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakiendelea na vikao vya Bunge hilo,vinavyoendelea leo Mjini Dodoma.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakibadilishana mawazo nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo.
The mdudu,kuna picha inajionyesha kabisa ya kwamba mama kaambiwa hapa hakuna UDINI wala MNYANYASIKO wa KIJINSIA hapa tupige kazi tuliotumwa na watanzania wenzetu ili tupate KATIBA yenye jita kwa taifa na vizazi vijavyo na sivinginevyo au ww mwenzangu unaonaje? Mama kashusha kicheka cha furaha ilioje na kumjibu natamani mijibaba yote kule ndani iwe na mawazo kama yako,maana hayo yote ulioyasema ndio hayo hayo nilitaka kukwambia haki yamungu naapa kwa mungu,ila hao wa poshozzz walegee wawe na uzito kama sufi,the mdudu nimeipenda sn sn hii picha,mungu ibariki tanzania yetu.angalizo kwa wajumbe wote toka kwangu hivyo viti msiviegamie mviogope kama wengine wanavyoonekana la sivyo MTAUCHAPA USINGIZI
ReplyDelete