Maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kigamboni katika mkondo wa Kurasini (Kurasini Creek) ulioanza mwaka juzi na kutegemewa kukamilika baadaye mwaka huu. Mradi huu wa daraja la kuning'inia, uliobuniwa na kampuni ya Arab Consulting Engineers na kujengwa na wakandarasi kampuni za China Railway Jiangchang Engineering (T) Ltd na China Major Bridge Engineering Company , unamilikiwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)  kwa asilimia 60 na Serikali asilimia 40, kwa gharama ya dola milioni 136 za Kimarekani. Utapokamilika utakuwa njia mbadala  ya safari za kwenda na kurudi maeneo  Kigamboni ambapo sasa zinatumika pantoni eneo la Magogoni Ferry

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Ahsante Kikwete!

    Nilifanya makosa makubwa sana kuigharimu Serikali ya Tanzania kuomba Pasipoti mwaka 2005.

    Baada ya Ujenzi wa Daraja hili kukamilika nadhani sina sababu ya kwenda Ulaya ama Marekani, maana Kikwete ametuletea Majuu hapa hapa kwetu!

    MWAKA HUU NITAIRUDISHA PASIPOTI IDARA YA UHAMIAJI!

    ReplyDelete
  2. Haiwi haiwi daraja limekuwa hii itasaidia sana usafiri wa kwenda na kurudi Kigamboni

    ReplyDelete
  3. Watanzania imefika wakati sasa tuache kuilamu serikali maana nayo kuna mazuri imetufanyia.

    Tunaiomba serikali yetu iendelee na mipango ya maendeleo ya namna hii

    ReplyDelete
  4. Dola 136 tu!!!!??? Kaka misupu Tafadhali.

    ReplyDelete
  5. Mdau wa 3 wengi wanaolalamika dhidi ya Serikali hawana Takwimu wala Ushahidi wa wanacholalamikia.

    Wengi inajulikana hawafuatilii mambo na kama wanayapata mambo ni kupitia Redio Mbao.

    Hivi hapa ninavyo andika nipo kwenye Inteneti ya Maktaba Kuu ya Taifa (Taasisi ya Kiserikali)hapa Dar Es Salaam ambapo mtandao wake ni Babu kubwa viwango vya juu ina Kasi ajabu, na bei ya chini kwa saa Tsh.500 !, kitu ambacho hakuna mtoaji Huduma Binafsi kwa siku za sasa atakupatia Mtandao kwa bei hiyo.

    Hivyo hii pekee kuwepo na Huduma za INTENETI Maktaba Kuu ya Taifa , hebu nielezeni kwa sisi tuliosoma miaka hiyo ya 1990's chini huko haya tuliyakuta hapa Maktaba?,,,Thubutu !!!, sisi tulicheza na vumbi za kwenye Makabati ya Vitabu, kusoma vitabu vizuri kwa Foleni vitabu tunawekeana foleni!!!

    Udhaifu mwingine kwa sisi Watanzania ni kutokupenda Kusoma!, mfano hapa Maktaba Vitabu vimejaa vumbi!!!, Makarani wanafanya kazi ya kufuta mavunmbi kila siku huku Watanzania wakiwa buzy huko Mitaani ktk mabishano Maskani na Vijiwe vya Kahawa!

    Watu hata kusoma Magazetiya habari za maana hawasomi watu wansoma zaidi Magazeti ya Udaku na Michezo hivyo ni wazi kwa kutokuitumia INTENETI KAMA hii ya SERIKALI HAPA Maktaba Kuu ya Taifa YENYE VIWANGO VYA KIMATAIFA kuto peruzi Mtandaoni na kutokusoma NI SAWA WATAKUWA DAIMA WANA ILALAMIKIA SERIKALI KWA KUWA HAWASOMI NA KUFUATILIA MAMBO KTK VYANZO VYA KUAMINIKA.

    ReplyDelete
  6. Wadau mimi kwa heshima kubwa kabisa Pasipoti yangu nitamkabidhi Raisi Kikwete atakapo kuwa anamaliza muda wake wa Uongozi akiwa atatuaga Watanzania, nikithibitisha ya kuwa kazi ameifanya na hivyo mimi sihitaji kuwa na Pasipoti kwa kwenda Ulaya na Marekani!!!

    ReplyDelete
  7. EBWANA EEEE Dar inang'ara !

    Kilicho bakia tufanye kazi kwa bidii tuweze kula Majuu tunayo hapahapa!

    Hivi hili Daraja si litakuwa kama lile la London-Uingereza kule Sussex ama la Los Angeles kule San Franscisco?

    ReplyDelete
  8. kilichonifurahisha ni kwamba kumbe watanzania tunajua ku appriciate kwenye mazuri thanx wadau wote mliompa hongera mr president kwa kweli kuna mambo mengine amejitahidi sana kwenye ukweli lazima tuuseme big up bro kikwete na magufuri katika anga hizo za magufuri hajakuangusha

    ReplyDelete
  9. Waoooo...ngoja nitafute kiwanja Kigamboni sasa...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...