Pichani juu ni baadhi ya wadau wa Soka waliokutwa hivi karibuni wakijisaidia kwenye masinki ya kunawia mikono kama waonekanavyo pichani.
Hapa baada ya kumaliza shughuli yao haoo wakaondoka,je wahusika wanalichukuliaje jambo hili lisilo la kiungwana kabisa ndani ya uwanja wa wetu wa mpira,ambao umejengwa kwa gharama kubwa,lakini kuna baadhi ya watu kama hawa wamekuwa wakiharibu maeneo na vifaa mbalimbali ya uwanja huo ikiwemo na kugeuza matumizi yake.

Ni mimi Mdau wa Soka la Bongo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. Jamani tatizo halitatuliwi kwa kulalamika bali kwa kuchukua hatua siyo lazima TFF bali hata wewe peleka picha hizo polisi Chang'ombe ili hawa jamaa wakamatwe mara moja. lakini tatizo ni nini hakuna vyoo ama? ni ujinga tu.

    ReplyDelete
  2. Kama wanaume wangejisaidia wakichuchumaa haya yasingewezekana. This is a gender based offence - wanaume tu ndio wahusika.

    ReplyDelete
  3. nashauri itumike mbinu inayotumiwa na manispaa ya moshi mjini ... iwekwe faini kwa yeyote atakaye hujumu miundombinu ya uwanjani ..yaani.. ukimkuta anaye hujumu ukamkamata na kumpeleka kwa uongozi; mtuhumiwa atatozwa kiasi cha Tsh.50,000/- au zaidi, 20,000/- ibaki kwa uongozi wa uwanja na 30,000/- apewe aliye mkamata au zaidi kulingana na kiwango kilichotozwa na risiti itolewe.

    ReplyDelete
  4. Ni bora upewe n'gombe 1000 uwaongoze kuliko kupewa watanzania 1000 kuwaongoza ! wanakatisha tamaa,

    Sijui tumelogwa na nani! sijui lini tutastaarabika, ndio maana watu wengine wanaona bora kufa maskini wakae ughaibuni kuliko kuja kwenye nchi yenye karaha namna hii.

    Nenda Mombasa, panton watu wooote wanakaa juu lakini apa kwetu watu wanashindana na magari na pikipiki balaa tupu!

    Kodi zinaliwa bila mpangilio, hali za wanacnhi zinazidi kuwa duni! yaani hata sijui niseme vipi aaah!

    ReplyDelete
  5. mm nashauri ziwekwe camera kwenye vyoo na maeneo mengi ya uwanja na kuna sheria na tangazo liwekwe ukifanya makosa haya faini yake elfu hamsini watu wataacha

    ReplyDelete
  6. OMG.Asante sana kwa kuliona hili mdau ingawa siyo la jana wala juzi.Hili suala si la TFF peke yake.Suala la usafi/Ustaarabu ni suala mtu binafsi kuanzia nyumbani kwake+Elimu na uelewa mdogo.Dawa ni kuhakikisha CCTV camera zinafanya kazi na hawa wanakamatwa na kufikishwa kwenye mkono wa sheria(adhabu kali),tatizo vyombo vinavyohusika vina maneno lakini havina sauti,vina upeo lakini havina macho.Ni Aibu

    David V

    ReplyDelete
  7. Ukiwaita minyani isiyokwa na ustaarabu wataanza kulia.Dawa yao ni ndogo tu, kamata halafu chapa fimbo thelathini, halafu watumie midomo yao kusafisha maskinki, hawatarudia tena, "unaweza kumtoa nyani toka porini, lakini huwezi kulitoa pori kutoka kwa nyani".

    ReplyDelete
  8. Elimu pia juu ya ustaarabu inahitajika, mnaweza kulaumu tu lakini sikazi hao wenzenu wanafikiri kuwa hivyo ni vyoo vya kisasa!! jamani si kila mtu kwake ana choo cha kisasa na masinki ya kidhungu kama hayo; na wengi wao hata kupata bahati ya kumtembelea mwenye km hivyo hamna, kwani ndungu wote nyumbani kwao, marafiki, majirani etc ni vyoo vya shimo vya nje, na bafu la nje; sinki la nini na atalijua wapi?? au alione wapi zaidi ya uwanja wa mpira?? sasa usipomwelewesha kuwa hilo ni la kunawia mikono na si kunanihii, basi mambo yatakuwa mazuri. Awareness itolewe, kwamba hayo masinki kazi yake nini period.

    ReplyDelete
  9. Napendekeza baada ya CCTV Camera kudaka Taswira kama anavyo pendekeza Kiongozi David V. hapo juu WARUSHWRE LIVE KATIKA TBC 1 (Televisheni ya Serikali ili nchi nzima na familia zao majumbani iwashuhudie wakifanya ujinga wao wanapokuwa Mpirani Uwanja wa Taifa) halafu ndio wapelekwe Mahakamani kwenye Sheria!!!

    ReplyDelete
  10. Wapimwe akili kwanza!

    Mnajua wajameni mtu anaweza kutoka nyumbani kwake ama kazini kuelekea Uwanja wa Taifa akiwa na akili kamili!, lakini kwa mapungufu ya ubinaadamu iukichangiwa na Mabange, Madawa ya Unga na Mapombe inawezekana mtu huyo akikaribia Geti la kuingia Uwanja wa Taifa anakuwa hana akili timamu anapata Kichaa na amegeuka Mtambo bin Taahira !!!

    Ubinaadamu kazi!

    ReplyDelete
  11. Hivi Waheshimiwa mnao jisaidia hapo ktk Masinki, mfano mimi mkinikjaribisha majumbani kwenu halafu na mimi nikajisaidia ktk Sinki tena la Meza ya chakula sebuleni mtafurahi?

    Thubutu!!!

    Kwa watu kama ninyi nadhani nitatoka marehemu kwa kipigo!

    Lakini kwa ninyi wawili ktk hayo Masinki ya Serikali ya Kikwete ahhh mnaona ndio pa kutolea haja ndogo!

    ReplyDelete
  12. Waadhibiwe ilim iwe fundisho!!!

    ReplyDelete
  13. Ukosefu wa ustaarabu kama huu tunasubiri kuuona ktk ndani ya Mabasi yaendayo Kasi Darisalama DART yakianza huduma Jijini hivi karibuni!

    Zifungwe CCTV Camera kuwaumbua watu wa namna hii!

    ReplyDelete
  14. jamani hawa ni wanyama kisayansi binaadamu si mnajua tumo kwenye kundi hilo.
    hatukuwekwa kwenye fungu la wanyama kwa kuwa tuna pembe au mikia tumewekwa kwa sababu na sisi hazitutoshi kama walivyo wanyama wengine.
    tunauwana ovyo,tunajamiiana ovyo na tunajikojolea ovyo.
    someni sayansi vema msihadaike na kupiga pasi nguo mkafikiri nyinyi watu.
    mimi sishangai na haya kwani nimeona mengi ndio maana nakubali kuwa mimi mnyama.
    kazi kwenu manaongangania kuwa nyinyi sio wanyama.
    mdau.
    porini, iringa.

    ReplyDelete
  15. akitekt na injinia ndo wabovu kujenga vyumba vichache. Hata ajali huko barabarani ni hao bali nyie mwalaumu dereva na wapita njia.

    we umebanwa halafu vyumba vyote vimejaa sasa uloweshe nguo?

    ingekuwa porini utachimba dawa.

    tena hao wastaarabu kwa sababu hawakukojoa sakafuni bali kwenye njia ya maji taka.

    wakati mwingine msitoe lawama hovyo.

    ReplyDelete
  16. Ndugu zangu wa Bongo,David V na Anonymous#5, kusema kweli hatuwezi kuweka Camera vyooni, kwa sababu ya usiri wa mtu na ni haki ya mtu kufanya yake bila kuangaliwa. Tuombe tu, watu wawe waastrabu wenyewe.
    Lakini nawaunga mkono, ili swala la vyoo vya uwanja wa Taifa kuharibiwa na mie nimeliona na nimelisema sana, na hata miaka ya karibuni nilienda kuangalia kombe la Kagame na wageni fulani, ilikuwa aibu. Niliwaambia hata viongozi wa TFF wakati ule. Vile vile niliandika kwenye wall ya Facebook yangu kama hivi. Nashangaa, Ni kweli wewe MZALENDO, MTANZANIA, MPENZI WA MICHEZO, unatoka kwako kuja kuvunja vifaa uwanja wa Taifa bila aibu!!? (Kuna jamaa wengine wakasema nikae kimya kwani nalipa taifa sura mbaya kwa wageni.
    Mio naona suluisho, ni (1)elimu, tufundishe uzalendo, watu wapende vitu vya jamii kwani ni vya kwao. (2)Uwanja wa Taifa wangewaajili watu wanaotoa huduma ya usafi vyooni ili watu wanaoingia wanatoa kama shukrani(tips), lakini vile vile hawa watu wanaangalia usalama wa vyoo. (3). nakubalina karibu nyie wote hapo juu, TFF inaweza kuomba serikali ikaweka maaskali, hakimu, na mahakama ya muda hapo hapo. Ukikamatwa unavunja sheria kama hizo picha hapo juu ni hukumu na faini ya hapo hapo.
    Mwisho naomba Watanzania tujipende, yaani utu na heshima viwepo jamani.

    ReplyDelete
  17. Kama vipi hii mada ipandishwe juu tena.Napenda kumjibu rafiki yangu mdau anayesema CCTV camera kufungwa sehemu kama hizo zitaharibu usiri wa watu.Ni kweli kabisa.Lakini CCV za sehemu kama hizi zinakuwa na watu wake special wa kufungua hiyo clip kama itahitajika kufanya hivyo.CCTV zinafungwa hata kwenye vyumba vya mahoteli lakini wenye hoteli camera zingine hawana access nazo. Kuna camera fulani(kama za humu) watu wa uwanjani wanakuwa hawana access nazo hadi pale kunapokuwepo na tukio la hatari sana.Niliwahi kusafiri na mke wangu kwenda Ulaya,chumba tulichofikia hotelini kilikuwa na CCTV camera ambayo watu wa hotelini hawana access nayo ila kama kuna ISSUE ya hatari vyombo vya dola vinaifungua clip yake.ILIBIDI tuzime taa,sijui kama ilisaidia.(Nadhani kwa wakubwa mnanielewa).Dunia ya leo haina tena Privacy rafiki yangu,watu tumegeuka kuwa kama "wanyama pori".

    David V

    ReplyDelete
  18. Wasimamizi wa sheria wanalegeza sana ndio maana nchi na wananchi hakuna adabu wala kuogopa kutenda kosa au kuvunja sheria za nchi.

    ReplyDelete
  19. Kwa kweli inasikitisha sana kuona vitendo kama hivi visivyo vya kistaarabu vinafanyika ndani ya uwanja wetu wa taifa uliojengwa kwa gharama kubwa.Naliomba jeshi la Polisi na uongozi wa chama cha mpira, kwa kutumia picha hii wawasake hawa wahalifu na kuwafungulia mashataka dhidi Yao.Picha zao zisambazwe kuwa wanatafutwa na chama cha mpira kitangaze zawadi nono kwa atakaetoa taarifa za kupatikana kwao ili wakipatikana basi adhabu Yao iwe fundisho kwa wengine.
    MDAU WA MICHEZO-

    ReplyDelete
  20. USTARABU ULIANZIA PWANI

    ReplyDelete
  21. So what kama ulianzia pwani? Wakati huko pwani wanatumia vyoo vya shimo usishangae hao ni watu wa pwani wanafikiri masinki ni choo!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...