Ujasiriamali ni jambo lililojema miongoni mwa jamii. Watu wengi wamekuwa wakilalamika kukosa vitu vya kufanya ili kuweza kujipatia kipato na kuacha kuwa tegemezi kwa wazazi au waume na hata wakati mwingine wake zao. Wana dada wawili marafiki ambao kwa bahati majina ya ubini ya wazazi wao yanafanana na wao kuamua kujiita ndugu,  Joan Joseph Massawe (pichani kulia)  na Angel Fabian Massawe wao kwa kuliona hilo waliamua kuanzisha bishara ambayo itawapatia kipato cha ziada mbali na ajira zao nma kuwasaidia katika masomo yao.

Wakiuambia mtandao huu wa Father Kidevu Blog kuwa wao ni wasomi na wameamua kuopika vitafunwa vya aina mbalimbali na kuviuza na pia wamekuwa wakifanya hivyo katika tafrija mbalimbali kwa kupika bite. 
Muiongoni mwa vitu ambavyo leo viilivuta FK Blog hadi katika meza ya wana dada hao 'The Ladies' iliyopo katika maonesho ya Tamasha la Mwanamke na Akiba ndani ya Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam ni vitumbua. Yes Vitumbua hivi hivi, maana ni vikubwa na vinamvuto. Lakini pia katika meza yao kulikuwa na vitu vingi kama chapati za maji na kusukuma, sambusa, kababu, kalimati, na kalimati.

Wanadada hawa ni mfano wa kuigwa kwa namna ambavyo waliamua kubuni biashara hiyo. Na niwazi kuwa hata hapo baade wakiwa na kampuni kubwa ya biashara hii sitaweza jkushangaa.
 Pichani ni Angel na Joan wakiwahudumia wake wa viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mke wa Makamu wa Rais mama Asha Bilali aliyekuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa tamasha la Mwanamke na Akiba.
 Angela na Joan wakimhudumia mama Asha Bilali vitumbua hivi ambavyo leo navizungumzia.
 Hakika kila mama aliyepita katika banda hilo hakuacha kununua kitafunwa.
 Vitumbua hivyoooo kazi kwenu wana dada hawa wanapatikana Oysterbay barabara ya Bongoyo.  
MAWASILIANO ZAIDI KWA WENYE UHITAJI: 
+255 713 185065 AU +255 652 035652

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Ni sawa katika kujikwamua kiuchumi lakini jee wanafuata kanuni za afya kama inavyoagizwa na wizara ya Afya?Jiko liwe safi,vyombo viwe safi maji yawe safi, mainzi wasiruhusiwe kutuwa,la si hivyo ndio yaleeeeeee!This is just precaution.

    ReplyDelete
  2. Uzuri wa kuona sio hoja jee walaji mmevionaje vitumbua? Mafuta hayakutopea? Jee havina mchanga viko laini kama sufi ,amaje twambieni ili tuvisifu saidi na kuchangia zaidi. Biashara isifiwayo ndiyo ivamiwayo!!

    ReplyDelete
  3. Vitumbua ni Vitamu sana Kwa sababu vina Mafuta na Sukari.

    Lakini Ndivyo vinafanya dada zetu na Mama Zetu kuwa Wanene sana.

    Wanaharibu sana Afya Zao na Miili kuwa Mikubwa sana Kwa Maandazi, machapati, Na Vitumbua.

    Tafadhali kula kwa ungalifu

    ReplyDelete
  4. Hizi ndio shughuli za kufanya!

    1.Ndio jibu sahihi la kuondokana na umasikini na kupata hali bora, Uchumi sio mpaka ufanye biashara za Mitaji Mikubwa sana.

    2.Uajira nzuri ni ile uipatayo kutoka katika sehemu yako ama bidhaa za eneo lako mfano maandalizi haya ya bidhaa za vyakula.

    3.Kwa msingi wa kazi kama hizi hakuna sababu ya kujenga Fikra juu ya Uchumi wa Madawa ya Kulevya nakuwa kazi za halali kama hizi na Vipato vyake hata Mwenyezi Mungu amevibariki sana!!!

    ReplyDelete
  5. Tatizo ya vitafunwa hivyo ni mafuta hata kama ni vitamu vyakula vya mafuta mengi, chumvi au sukari nyingi siyo vizuri kwa watu wenye zaidi ya miaka 40

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...