Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Hassan Bendeyeko akitoa ufafanuzi juu ya utekelezaji wa miradi ya TASAF katika halmashauri za wilaya na Manispaa Mkoani Ruvuma kwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF Abbas Kandoro, ambaye ameongoza wajumbe wa kamati hiyo kukagua miradi iliyotekelezwa na TASAF kwa kushirikiana na wananchi katika Mkoa wa Ruvuma.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF Abbas Kandoro akisisitiza jambo kwa viongozi (hawapo pichani) wa halmashauri ya wilaya ya Songea na Manispaa ya Songea baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa miradi ya TASAF katika awamu ya pili.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF Abbas Kandoro akielekea kukagua mradi wa maabara katika shule ya sekondari ya Mfaranyaki katika Manispaa Songea. Katika shule hii imetekelezwa miradi mitatu ambayo ni Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa, maabara mbili na jengo la utawala vilivyogharimu shilingi milioni 197
Wajumbe wa kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukagua miradi ya TASAF katika shule ya sekondari ya Mfaranyaki Mjini SONGEA. Picha na Gerson Partinus Msigwa, Songea
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...