Mwenyekiti wa kamati ya mashinda ya Tunzo ya Ushairi nchini Tanzania Ibrahim Seushi akizungumza wana wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Tuzo hizo mapema hivi karibuni. Tuzo hizo zitaitwa Ebrahim Hussein ikiwa ni kumuenzi nguri na mkongwe huyo wa mashairi hapa nchini.
Jaji Kiongozi wa Tuzo za Ebrahim Hussein Profesa Mugabyo Mlinzi Mulokozi akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa tuzo hizo mapema hivi karibuni.
Profesa Ebrahim Hussein (katika) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa tuzo za mashairi zilizopewa jina lake ikiwa ni kuenzi mchango wake katika tasnia hiyo mapema hivi karibuni.
Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Hajaty Shani Kitoga akiimba shairi la Wakati Ukuta ambaole ni moja ya kazi za Profesa Ebrahim Hussein wakati wa uzinduzi wa tuzo za mashairi zilizoanzishwa mapema hivi karibuni.
Mkurugenzi wa Mkuki na Nyota Publisher Bw. Walter Bgoya akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa tuzo za mtunzi wa mashairi ambapo kampuni hiyo ndiyo muendeshajio wa mashindano hayo.
Profesa Ebrahim Hussein (katika) akiwa katika picha ya pamoja na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa tuzo za mashairi zilizopewa jina lake ikiwa ni kuenzi mchango wake katika tasnia hiyo mapema hivi karibuni. Picha zote na Frank Shija - WHVUM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Oh the author of Kinjekitile na mashetani. Anastahili kukumbukwa kwa kweli. ni mmoja wa waandishi wazuri sana wa kiswahili. Tunashukuru kwa kututumbuiza kupitia mashairi na riwaya.

    ReplyDelete
  2. Humu mbona metukhini, kwa hilo nalalamika, Ebrahimu Huseni, beti zake mngeweka,
    Japo walo vipembeni, zighani ngefarijika,
    Wahusika hongereni, 'Tuzo' wazo muafaka.

    ReplyDelete
  3. Ahsante Sana Michuzi kwa kutuletea habari za profesa Ebrahim Hussein.Kazi yako ni nzuri Sana maana hizi habari ni adim Sana.Profesa ametunga vitabu vingi Sana katika lugha tofautitofauti kikiwemo kifaransa,kijerumani,English na kiswahili.Baadhi ya vitabu ni Kama vofuatavyo African Literature,Wedding,Demons,Time is Wall..............Anastahili tunzo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...