Mwaka 2009, wazo jipya lilizaliwa. Wazo la kuwa na tuzo zitakazopatikana kwa mchakato wa wazi utakaotokana na mapendekezo ya watu wenyewe ya kuchagua mastaa wa michezo, muziki, filamu au vipindi na watangazaji wanaopendwa zaidi. Wazo hilo liliendelea kuboreshwa na mwaka huu (2014), limeiva na liko tayari kutoka kwenye hatua ya wazo la kichwani, na kuwa tukio lenyewe.
"Nilizisajili na kuanzisha mwaka 2009 ila kutokana na mipango na malengo ya kampuni niliamua kuziweka kwanza hadi sasa," anasema Mwenyekiti wa Bongo5 Media Group, Luca Neghesti.
"Sasa hivi tumeshuhudia ukuaji katika tasnia mbalimbali na tumeona ni wakati muafaka wa kuwatunuku wale wanaopendwa na wananchi, kuwapatia tuzo pamoja na zawadi ya fedha taslimu milioni 1" ameongeza.
Tofauti na tuzo zingine, tuzo za watu hazitafuti ubora bali zinalenga wanaopendwa zaidi na tuzo hizi hazitajikita katika tasnia moja peke yake.
Kwa kuanzia, tuzo hizi zitatolewa katika tasnia ya burudani inayojumuisha filamu na muziki. Pia zitaiangazia sekta ya utangazaji kwa kuwatunuku watangazaji na vipindi vinavyopendwa zaidi na watu nchini huku pia mwanamichezo bora (soka, basketball, ndondi na michezo mingine) naye akipewa nafasi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...