Katibu tawala wa mkoa wa dodoma Ndg. Rehema Madenge amemtaka Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya mpya ya Chemba mkoani Dodoma na timu yake ya wataalamu kuweka mara moja utaratibu wa kutembelea vijijini mara kwa mara kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwenye wilaya hiyo mpya.
Agizo hilo lilitolewa mapema wiki hii wakati wa ziara ya timu ya wataalamu kutoka sekretarieti ya mkoa wa dodoma wakiongozwa na katibu tawala hiyo walipotembelea wilaya ya chemba kukagua utekelezaji na usimamizi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa wilayani humo.
Matokeo ya ziara hiyo yalionesha kuwa pamoja na sababu na changamoto nyingine, kudorora kwa utekelezaji wa baadhi ya miradi unachangiwa na utamaduni wa viongozi na wataalamu kutotembelea vijijini mara kwa mara kukagua utekelezaji wa miradi hiyo ya maendeleo.
Katibu tawala huyo ametahadharisha tabia ya kutegemea taarifa za kwenye makaratasi vitabuni kwani mara nyingi zinaonesha hali ni nzuri lakini utakapokwenda moja kwa moja kkutembelea miradi utafahamu hali halisi na hatua ya miradi na changamoto zake.
Kwa mujibu wa ziara hiyo iliyofanyika ilibaini baadhi ya miradi kama ule wa maji (ujenzi wa tank na miundombinu ya usambazaji) kijiji cha kelema kuu kuwa na matatizo katika utekelezaji wake ambapo mkandarasi Juin Construction alitakiwa kukamilisha mradi oktoba 20, 2013 lakini hadi sasa bado mradi huo haujakamilika na unaonesha wasiwasi kwenye viwango.
Baadhi ya matatizo mengine yaliyobainika kwenye ziara hiyo ni pamoja na uwezo mdogo wa wakandarasi waliopewa miradi hiyo kujenga, kwani wakati wanaomba kazi za miradi,walionesha wanauwezo mkubwa lakini wakipewa miradi kujenga wanaonesha hali ya kusuasua.
Nae mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya Chemba Ndg. William Mafwele amesema halmashauri hiyo ni mpya imeundwa kufuatia serikali kuanzisha wilaya mpya miaka ya hivi karibuni, changamoto wanayokumbana nayo ni pamoja na mikataba mingi ya utekelezaji miradi ya maendeleo pamoja na fedha vilisainiwa na vinasimamiwa utekelezaji wake na halmashauri mama ya wilaya ya kondoa iliyounda wilaya ya chemba hivyo wao wanakosa nguvu za usimamizi.
Sekretarieti ya mkoa wa dodoma imeahidi kuishughulikia changamoto hiyo na kuagiza kwa sasa wilaya hizo mbili chemba na kondoa zishirikiane kwa karibu katika utekelezaji wa miradi, usimamizi na hata ufuatiliaji wake.
(HABARI NA PICHA NA JEREMIA MWAKYOMA OFISI YA MKUU WA MKOA WA DODOMA)
Tanki la maji ambalo bado ujenzi wake haujakamilika wakati muda aliopewa mkandarasi kutekeleza umeshapita, Mradi huu upo kwenye kijiji cha Kelema Kuu wilayani Chemba Dodoma, wanaoonekana ni wataalamu wa maji wa wilaya ya chemba wakati wa ziara ya pamoja na wataalamu wa sekretarieti ya mkoa wa dodoma walipotembelea miradi ya maendeleo kwenye wilaya hiyo.
Matofali yaliyotengenezwa kwa ajili ya ujenzi wa tanki kubwa la maji lenye ujazo wa lita elfu hamsini ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa maji wa kijiji cha Kelema Kuu wilayani Chemba Dodoma, ziara ya wataalamu kutoka Sekretarieti ya mkoa wa dodoma iliyowashirikisha wataalamu na watendaji wa wilaya ya chemba ilibaini baadhi ya matofali haya kuwa na nyufa jambo llililoonesha wasiwasi wa ubora wake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...