Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(Watatu kushoto) akiwa pamoja na Viongozi wa Ikulu SACCOS wakati walipokwenda kujitambulisha na kukabidhi ripoti ya utendaji ofisini kwake ikulu jijini Dar es Salaam leo.Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa SACCOS hiyo Bwana Theofrid Kikombele, Wapili kushoto ni Katibu wa SACCOS hiyo Bwana David Kivembele na kulia ni mshauri mkuu wa SACCOS hiyo Bwana Joseph Sanga. 
Viongozi wa Ikulu Saccos wakiwa kwenye mkutano na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ofisini kwake ikulu jijini Dar es Salaam leo.

Na Freddy Maro. Ikulu.

Uongozi Mpya wa ikulu SACCOS leo umejitambulisha rasmi kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, ikulu jijini Dar es Salaam na kukabidhi ripoti ya utendaji ya SACCOS hiyo.

Waliojitambulkisha kwa Katibu Mkuu Kiongozi ni pamoja na Mwenyekiti wa Ikulu SACCOS Bwana Theofrid Kikombele,Makamu Mwenyekiti Bwana David Kivembele na Mshauri Mkuu Bwana Joseph Sanga.

Akizungumza mara baada ya kujitambulkisha, Mwenyekiti wa SACCOS hiyo Bwana Theofrid Kikombele alisema uongozi huo umepanga mikakati madhubuti ya kuiendesha SACCOS hiyo kwa uwazi na ufanisi zaidi ikizingatia kutenda kazi kwa weledi na kuwahamasisha wafanayakazi wengi zaidi kujiunga.

Mkakati mwingine, alisema Bwana Kikombele ni kwa SACCOS hiyo kuanzisha vitega uchumi mbalimbali kwa lengo la kupanua mtaji ili kuweza kuwahudumia vyema wanachama wa SACCOS hiyo kwa kuwawezesha kukopa zaidi kwaajili ya shughuli zao mbalimbali za kujiletea maendeleo.

Wakati wa mkutano huo kati ya Katibu Mkuu na Uongozi wa Saccos hiyo Viongozi hao walikabidhi ripoti ya utendaji wa SACCOS hiyo na walimuomba Katibu Mkuu Kiongozi kujiunga na SACCOS hiyo, ombi ambalo aliliafiki na kuahidi kutoa ushirikiano kuboresha SACOSS hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...