Mwenyekiti wa Tancraft, Elihaika Mrema akizungumza na waandishi wa habari umuhimu wa jumuiya kubwa za wafanyabiashara na pamoja na serikali kuwaunga mkono wajasirimali wanawake nchini, Kushoto ni Esther Kasenga Msaidizi wa Katibu, Kulia Mweka hazina wa Chama cha Tancraft, Bi.Louise Judicate na Wapili kulia ni Katibu wa Tancraft, Bi. Vicky Shayo.
Na Damas Makangale
WAMILIKI Wote wa maeneo ya biashara nchini wameombwa kutoa nafasi ya maeneo ya biashara kwa wajasirimali wanawake ili kumkomboa mwanamke kutoka katika dimbwi la umaskini na utegemezi. MOblog inaripoti.
Akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wajasirimali wanawake jijini Dar es Salaam leo mchana, Mwenyekiti wa Tanzania Handcraft Association (Tancraft), Elihaika Mrema amesema kuwa wanawake wafanyabiashara wadogo wana matatizo na changamoto kadhaa mojawapo ni maeneo ya kuuzia bidhaa zao.
Pichani juu na chini ni Baadhi ya Wajasiriamali Wanawake wakifuatilia hotuba ya mwenyekiti wa TANCRAFT Bi. Elihaika Mrema alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika jengo la Biashara la DAR FREE MARKET lililopo barabara ya Ali Hassan Mwinyi karibu na Ubalozi wa Kenya nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...