Mchora vibonzo na Mratibu wa Wafanye Watabasamu, Nathan Mpangala, akiongea na baadhi ya watoto wa Kituo cha SOS Children’s Villages cha Dar es Salaam wakati wa ziara ya mafunzo ya uchoraji katika kituo hiko, Juzi. Ziara hiyo iliyohusisha wachoraji na marafiki kadhaa ililenga kuibua vipaji na kuwatabasamisha watoto.
Mchora vibonzo Abdul King O ‘Kaboka Mchizi’, akitoa maelekezo ya jinsi ya ‘kutupia’ rangi kwa watoto wa SOS Children’s Villages, juzi.
Hili ndilo haswaaa lengo la Wafanye Watabasamu; elimu, ukuzaji vipaji na tabasamu.
Baadhi ya Makomredi wa Wafanye Watabasamu wakiwa wamekula pozi katika SOS Children’s Villages, juzi. Kutoka kulia, Godfrey ‘Mzee wa Beche’, Evaris Chikawe ‘Rasta bila masharti’ na Said Michael ‘Wakudata.’
Watoto wa SOS Children’s Villages cha Dar es Salaam, ‘wakizishambulia’ rangi wakati walipotembelewa na marafiki wa Wafanye Watabasamu, juzi.
Si umesema wewe ndiye mchora kibonzo ITV, tuoneshe?’ Baadhi ya watoto wa SOS Children’s Villages wakimdadisi mchora vibonzo Nathan Mpangala, mara baada ya zoezi la uchoraji kwisha.
Masikini tembo nae akakumbukwa na watoto.Picha zaidi bofya: https://www.facebook.com/pages/Wafanye-Watabasamu-Make-Them-Smile/140812046112398
These children are so cute....jamani kweli hawa watoto wanaishi vituo vya yatima wakati kuna watu mna uwezo mkuuubwa na hamna watoto...tubadili mindset zetu jamani...si mpaka mzungu ndio aje ku adapt.
ReplyDeleteMimi nina mpango wa kuchukua katoto ka kike kamoja maana nina madume ya mbegu tu...
Najua watu mtasema kachukue watoto wa nduguzo ulee....mtoto yatima ni wako ...wa ndugu yako wala si wako