Fredrick Mwakalebela mmoja wa wakufunzi watakaotoa mafunzo kwa wajasiliamali wa mkoa wa Iringa Feb 22
Mratibu wa semina ya ujasiliamali Anzawe Chaula akizungumza kuhusu semina hiyo ya februari 22 ofisini kwake. (Picha na Denis Mlowe)
======== ======= =========
WAJASILIAMALI KUPATIWA MAFUNZO IRINGA
Na Denis Mlowe,Iringa
KAMPUNI ya Vannedrick Tanzania limited (VTL) ya jijini Dar salaam kwa kushirikiana na Kituo cha Maendeleo,Haki na Utetezi TCDA cha mjini Iringa wameandaa semina ya ujasiliamali kwa wakazi wa manispaa ya Iringa zaidi 1000 inayotarajiwa kufanyika Februari 22 mwaka huu.
Akizungumza mratibu wa Semina kutoka TCDA Anzawe Chaula alisema lengo la kuandaa semina hiyo itakayojulikana kwa jina la Jukwaa la Wajasiliamali ni kuwakomboa wakazi wa mkoa wa Iringa kuondokana na umaskini na kuweza kujitambua katika utengenezaji wa malighafi mbalimbali.
Alisema katika semina hiyo itafanyika katika ukumbi wa Hallfare kutakuwa na mafunzo mbalimbali yanayohusu elimu juu ya kutafuta masoko ya bidhaa kwa wajasiriamali, jinsi ya kupata fursa za mikopo kutoka katika benki mbalimbali za ndani nan je ya nchi ya Tanzania.
Chaula alisema jukwaa la wajasiliamali litawafundisha wajasiliamali kutambua haki za kisheria katika biashara wafanyazo pamoja na kuratibu mafunzo ya mara kwa mara ya kuwajengea uwezo katika shughuli zao za kila siku.
“Kuna umuhimu mkubwa sana kwa wajasiliamali kupatiwa mafunzo ya mara kwa mara katika shughuli zao wazifanyazo kutokana na wengi wao kufanya biashara bila kuwa na elimu mtambuka ya kufanya kazi hizo na kuweza kujiongezea vipato hivyo sisi tutawapatia mafunzo hayo na naomba sana wajitokeze kwa wingi kuweza kuelimika juu ya ujasiliamali.” Alisema Chaula.
Aliongeza kuwa semina hiyo itawajengea uwezo wajasiliamali katika kutafuta na kutambua fursa mbalimbali zilizoko katika mkoa wa Iringa zikiwemo za utalii wa ndani ambao uko chini sana katika kutumia fursa hizo.
Aidha wajasilimali watapatiwa fursa ya kufungua biashara zinazoendana na wakati uliopo ukiwemo ujenzi wa barabara ya Iringa hadi Dodoma inayotarajiwa kukamilika mwakani kuweza kufungua miradi mbalimbali pembezoni mwa barabara hiyo na kuwatumia wanafunzi walioko vyuoni kujiongezea mapato.
Chaula alisema katika semina hiyo wakufunzi watakaoelimisha wajasiliamali ni Mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF), Dk Didas Lunyungu kutoka Dar salaam na Fredrick Mwakalebela na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...