Diwani wa Kata ya Kigamboni,Dotto Msawa akizungumza na wananchi wa Kata yake, wakati akifunga warsha ya siku moja iliyokuwa ikitoa mafunzo kwa kina Mama wa Kata hiyo,juu ya uhuhimu wa kujiunga na vyama vya VICOBA,iliyokuwa ikitolewa na Walimu kutoka Kituo cha Poverty Fighting Tanzania (PFT) cha Temeke jijini Dar es Salaam.
Wakinamama ambao ni wakazi wa Kata ya Kigamboni,wakimsikiliza kwa Makini Diwani wa Kata hiyo,Dotto Msawa (aliesimama) wakati alipokuwa akifunga warsha yao hiyo,ambapo amewataka kinamama hao kuwa na umoja na kupendana katika shunguli zao mbali mbali wazifanyazo,huku akiwaambia yupo pamoja nao na atakuwa akiendelea kuwasaidia katika mambo mbali mbali ya kimaendeleo.
Katibu Kata wa CCM katika Kata ya Kigamboni,Bi. Zahra Kayagwa akiwasalimia wakinamama wenzake wa Kata hiyo ya Kigamboni.
Sehemu ya Kinamama wa Kata ya Kigamboni,wakimsikiliza kwa makini Diwani wao,Dotto Msawa (hayupo pichani) wakati alipokuwa anazungumza nao alipokwenda kufunga warsha ya siku moja iliyokuwa ikitoa mafunzo kwa kina Mama wa Kata hiyo,juu ya uhuhimu wa kujiunga na vyama vya VICOBA,iliyokuwa ikitolewa na Walimu kutoka Kituo cha Poverty Fighting Tanzania (PFT) cha Temeke jijini Dar es Salaam.
Diwani wa Kata ya Kigamboni,Dotto Msawa (mwenye koti walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na wakinamama wa Kata yake hiyo,mara baada ya kufunga warsha ya siku moja iliyokuwa ikitoa mafunzo kwa kina Mama wa Kata hiyo,juu ya uhuhimu wa kujiunga na vyama vya VICOBA,iliyokuwa ikitolewa na Walimu kutoka Kituo cha Poverty Fighting Tanzania (PFT) cha Temeke jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...