Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Bw.Wayne Mcintosh, akizungumza na Wakuu wa Mercedes Benz kutoka Ujerumani na Wawakilishi wa Mercedes Benz Afrika katika mpango mkakati wa kubadilishana nao mawazo na uzoefu katika shughuli za biashara na masoko katika ukanda wa Afrika.
Wakuu wa Mercedes Benz kutoka Ujerumani na Wawakilishi wa Mercedes Benz ukanda wa Afrika ni kutembelea kampuni hiyo kubwa na ya siku nyingi ya magari hapa duniani na kuangalia aina mpya za bidhaa ambazo zipo sokoni na kupata kujifunza kazi mbalimbali za kijamii ambazo kampuni hiyo ya CFAO Motors inafanya hapa Tanzania.
Wakuu wa Mercedes Benz kutoka Ujerumani na Wawakilishi wa Mercedes Benz Afrika kutoka nchi za Rwanda, Sudan, Afrika Kusini na nchi zingine wamekuja nchi kwa ziara ya kikazi ya siku tatu na wamefanikiwa kujifunza shughuli mbalimbali za ufundi na utendaji kazi wa kampuni ya CFAO Tanzania.
Wakuu wa Mercedes Benz kutoka Ujerumani na Wawakilishi wa Mercedes Benz Afrika pia walipata fursa ya kuangali akarakana ya kampuni hiyo kwenye maeneo ya Vingunguti na kuona shughuli za ufundi kwa magari yao ambapo wateja ambao wanaharibikiwa na magari wanaweza kupata huduma hiyo kwenye karakana ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors, Charles-Edouard CAMBOURNAC akitoa maelezo kwa Wakuu wa Mercedes Benz kutoka Ujerumani na Wawakilishi wa Mercedes Benz Afrika.
Wakuu wa Mercedes Benz kutoka Ujerumani na Wawakilishi wa Mercedes Benz Afrika wakitembelea eneo linalotoa huduma ya kutengeneza kwa teknolojia ya hali ya juu magari ya wateja wa kampuni hiyo pindi yanapopata hitilafu. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...