Na Abdulaziz Video,Mnazi Mmoja ,Lindi.
Sekta ya Habari Imetakiwa kutoa elimu zaidi ya ukatili wa Kijinsia ili
kujenga Taifa lenye amani kwa wananchi Bila kujali Jinsia ,Dini na
kabila.
Wito huo umetolewa na Dr Monica Mhoja , Naibu Mkurugenzi wa mradi wa
Champion unaofadhiliwa na Usaid alipokuwa akitoa mada katika warsha ya
wanahabari wa Mkoa wa Lindi inayoendelea katika Ukumbi wa Sakina Mnazi
mmoja Manispaa ya Lindi.
Dr Mhoja amebainisha kuwa sekta ya habari ina wajinu mkubwa kwa
kushirikiana na serikali na mashirika yanayotoa elimu juu ya
Unyanyasaji kijinsiaNchini ili kuwapa mwanga jamii kuweza kuchukia
vitendo hivyo ambavyo ni kinyume na haki za Binadamu.
Wanahabari ni jukumu lenu kutoa hii kwa kuwa mnayo nafasi na fursa
kubwa ya kuelimisha kwa kuwa vitendo hivyo vinaongezeka kila siku
ikiwemo kupigwa,Ukeketaji na ndoa za utotoni ili kuondoa ubaguzi na
ukatili huo na hivyo kupitia warsha hii matarajio ya Shirika la
Champion ni kuondoa hali hizo kwa kupitia vyombo vya Habari ndio maana
tumewakusanya kuwapa elimu,Alimalizia Dr Mhoja.
Lengo la warsha hiyo ni kuwajengea Uwezo na Uelewa wa sheria na sera
za Nchi zinazohusisha masuala ya ukatili wa kijinsia.
Warsha hiyo pia Inaendeshwa na Ofisa mradi mwandamizi wa kutoka
kitengo cha mawasiliano mradi wa Champion,Bw Muganizi Mutta na tayari
mafunzo hayo yametolewa kwa Wanahabari wa mkoa wa Mtwara.
Naibu Mkurugenzi wa mradi wa champion akitoa mada kwa
wanahabari wa mkoa wa Lindi katika warsha inayoendelea.
Baadhi ya wanahabari wa Lindi wakiwa katika warsha ya ukatili
wa kijinsia inayotolewa na mradi wa Champion
Picha ya pamoja kati ya Naibu Mkurugenzi wa Mradi wa Champion
na wana habari wa mkoa wa Lindi waliohudhuria warsha kuhusiana na
sheria na Sera za ukatili wa kijinsia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...