Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe mwishoni mwa wiki alitembelea mradi wa maji wa dharura Karatu Mjini kuona utekelezaji wake.
Mradi huo mahsusi kwa ajili ya kukabiliana na upungufu mkubwa wa maji mjini Karatu unasimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Jijini Arusha (AUWSA).
Pia, Prof. Maghembe alitembelea Halmashauri ya Mji wa Karatu kuangalia hali ya upatikanaji wa maji na utekelezaji wa miradi ya maji wilayani humo katika programu ya vijiji 10 ya BRN.
Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa wakazi wa Karatu Mjini.
Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe akiwa na mwenyeji wake Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Felix Ntibenda (kulia) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Moses Mabula.
Mkurugenzi wa AUWSA, Inj. Ruth Koya akisoma Ripoti ya Maji ya Halmashauri ya Wilaya ya Karatu kwa Waziri wa Maji, Prof. Jumannne Maghembe.
Miundombinu ya mradi wa maji wa dharura Karatu Mjini.
Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe, akiangalia tanki la maji la mradi wa dharura wa Karatu Mjini, huku akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa AUWSA, Inj. Ruth Koya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...