Familia ya Nestory Mwombeki Rweyamamu ya Mt. Vernon New York imetoa ratiba fupi ya shughuli za msiba wa mama yao mpendwa Theonestina Rweyemamu kama ifuatavyo:
  • Kuaga Mwili wa Marehemu Mama Theonestina Rweyemamu itakuwa Jumatano tarehe 5 Februari 2014 kuanzia saa kumi jioni hadi saa mbili usiku. Mahala: Camelot Funeral Home, 174 Stevens Avenue, Mount Vernon, NY 10550;
  • Misa ya Kumwombea Marehemu itakuwa saa nne asubuhi siku ya Alhamisi tarehe 6 Februari 2014 kwenye kanisa la Moyo Mtakatifu au Sacred Heart Church. Mahala: 115 Sharpe Blvd., South Mount Vernon, NY 10550
  • Taarifa ya lini mwili wa Marehemu utasafirishwa kwenda Bukoba, Tanzania zitafuata baadaye baada ya mipango kukamilika. Mipango hadi sasa ni kumsafirisha Marehemu siku ya Ijumaa kwenda Tanzania.
Watoto wa Marehemu kina Doris, Steven, Emmanuel na Diana pamoja na familia nzima wanapenda kuwashukuru wote kwa kufika kuombeleza nao na kwa rambirambi zenu. 

Pamoja na ratiba iliyotajwa hapo juu, bado mnaweza kutuma rambirambi zenu kwao na kufika nyumbani kuwaona. Address ni: 40 East Sidney Avenue, Apt # 10C , Mount Vernon, NY 10550. Na namba ya simu ya nyumbani ni 914-667-6456.

Familia inahitaji kukusanya kiasi cha Dolla 10,000. Mpaka sasa kiasi cha Dolla 6,000 zimeshapatikana na kuna mapungufu ya dola 4,000. Uongozi unawaomba Wanajumuiya kujitolea ili kufikisha kiasi cha fedha kinachotakiwa. Kwa Wanajumuiya wa Queens na Brooklyn Mweka Hazina Msaidizi Dr. Temba atakusanya michango na kuiwakilisha kwa Familia ya Marehemu (na simu yake ni 646-489-6532) na kwa wanajumuiya wengine tunaomba mwasiliane na familia moja kwa moja au kwa kupitia simu zilizotajwa katika tangazo hili. Familia itashukuru msaada wowote wa kuwasaidia kuweza kufanikisha mpango wa kumsafirisha mama Theonestina Rweyemamu kwa kutoa chochote kwenye Bank of America, account number 483044166145 routing number 021000322 na jina kwenye account ni Doris Rweyemamu.

Kwa maelezo zaidi unaweza piga simu kwa wafuatao:

Emmanuel Rweyemamu 6462342418, Steven Rweyemamu 3028837971, Dr. Abbas Byabusha 9145847502, Doris Rweyemamu 6463799135.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa. Amen.

Uongozi-Jumuiya ya Watanzania New York.

Mwisho wa Tangazo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Poleni wanafamilia ya Rweyemamu tunawaombea mungu awape nguvu ktk kipindi hiki kigumu. By Mtanzania wa kawaida.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...