Waziri wa Maliasili na Utalii
Mhe. Lazaro Nyalandu akipongezwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Wanyamapori
Paul Sarakikya mara baada ya kumaliza mahojiano katika kituo cha BBC
jijini London alipokuwa akihudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Biashara
Haramu ya Wanyamapori. Kulia ni Katibu wa Waziri Imani Nkuwi.
Waziri wa Maliasili na Utalii
Mhe. Lazaro Nyalandu (kati) alipata fursa ya kukutana na Mwandishi wa
Gazeti la Daily Mail la Nchini Uingereza Martin Fletcher (kulia) na
kumfafanulia juu ya juhudi za serikali katika kupambana na ujangili
nchini. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Wanyamapori Paul Sarakikya.
Waziri wa Maliasili na Utalii
Mhe. Lazaro Nyalandu akihojiwa na Mtangazaji Shirika la Utangazaji la
Uingereza (BBC) Zawadi Machibya ambapo alipata nafasi ya kuzungumzia
juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali katika Vita Dhidi ya Ujangili
nchini na Changamoto zinazohitaji kuungwa mkono na Jumuiya ya Kimataifa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya
Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe. James Lembeli (kushoto)
akimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi wa Wanyamapori Paul Sarakikya (kulia)
jijini London walipohudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Biashara Haramu ya
Wanyamapori. Kati ni Katibu wa Waziri Imani Nkuwi.
Picha na Pascal Shelutete, TANAPA
Kazi nzuri Mheshimiwa Nyalandu!
ReplyDelete