Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu leo ametangaza kuwang'oa viongogo wa ngazi ya juu katika Idara ya wanyamapori akieleza kuwa ni kutokana na kutoridhishwa na utendaji wao. 


Ifuatayo ni Taarifa rasmi ya tamko la Waziri Nyalndu,  kama alivyolisoma leo:


Leo, TAREHE 24 Februari, 2014 Natangaza kuubadili uongozi wa Idara ya Wanyamapori ya Wizara ya maliasili na Utalii kama ifuatavyo: 

Ninamuondoa Profesa Alexander Songorwa katika nafasi ya Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori ya Wizara ya Maliasili na Utalii.  

Nachukua hatua hii kutokana na kutokuridhishwa kwangu na utendaji wa kazi wa idara hiyo katika mapambano dhidi ya ujangili yanayoendelea nchini.  
Aidha, hatua hii ni utekelezaji wa Azimio la Bunge lililotolewa tarehe 22 Disemba, 2013, lililotaka Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori kuwajibishwa kutokana na tuhuma za uzembe na ukiukwaji wa haki za binadamu katika Operesheni Tokomeza. 
Utekelezaji wa agizo hili unaanza mara moja, nami namteua Bwana Paul Sarakilya kukaimu nafasi hiyo ya Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori ya Wziara ya Maliasili na Utalii kuanzia sasa. 

Aidha, ninamuondoka Profesa Jafari Kidegesho katika nafasi ya Mkurugenzi Msaidizi wa Matumizi Endelevu ya Wanyamapori na kumteua Dr. Charles Mulokozi kuchukua nafasi hiyo. 

Hali kadhalika, ninamteua Bwana Julius Kibebe kuwa Mkurugenzi Msaidizi Uzuiaji – Ujangili na anachukua nafasi ya anayeenda kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Wanyamapori. 

Vilevile, Bibi Nebbo Mwina anaendelea kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo, Utafiti na Takwimu, na Bwana Herman Keiraryo anaendelea kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Uendelezaji wa Wanyamapori. Pamoja na Kitengo cha Uzuiaji – Ujangili nilichokitaja awali, hivi ni vitengo vya Idara ya Wanyamapori katika Wizara ya Maliasili na Utafiti. 

Nawaagiza kwamba Wakurugenzi na Wakuu wote wa kila Idara, kila Shirika, na Taasisi zote ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii kutengeneza viashiria muhimu vya utendaji kazi (Key Performance Indicators) na kukabidhi kwangu ndani ya siku 30 zijazo.  

Viashiria hivi ni hatua ya kufanikisha yafuatavyo, 1)  Malengo ya wizara, 2)  Uwajibikaji, 3) Uwazina 4) Ufanisi katika utendaji wa kazi za kila siku.  Ni sharti tutekeleze mikakati ya wizara katika mifumo inayopimika, tuweze kujipima natuweze kupimwa, natutumikie Taifa kwa uadilifu. 

Kwa mtumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii ikiwemo mimi mwenyewe, Lazaro Nyalandu, atapaswa kuzingatia na kutekeleza majukumu ya kazi kwa kuzingatia Kanuni za Mwenendo (Code of Conduct) ambazo zitapendekezwa na kupitishwa na Baraza la Wafanyakazi wa Wizara. 

 Baraza hili liwe limeitishwa na Katibu Mkuu wa Wizara kabla ya mwisho ya mwezi ujao.  Azma ya kanuni hizi ni kuwa na misingi bora ya utumishi, uwajibikaji, utu, usawa na haki katika utekelezaji wa majukumu yetu ya kila siku.
 Mungu ibariki Tanzania.
Asante.
 Lazaro S. Nyalandu (MB)
Wizara ya Maliasili na Utalii
24/02/2014

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. The mdudu,ndugu Nyalandu tumechoka kusikia watu wakiondolewa madarakani bila ya kuchukuliwa hatua KALI ili iwe fundisho kwa wengine,watu kama hao inatakiwa WAFIRISIWE MALI ZAO ZOTE walizozipata kwa njia ya UFISADI hii ni AIBU KUBWA kwa hiyo MIPROFESA kulihujumu taifa huku wakijua kabisa watanzania wengi wanateseka kwa umasikini na njaaa,,hivi rais aliposema anataka kuona maisha bora kwa kila mtanzania inamaana hamkumuelewa au mnamzarau na kuona kama kauli yake haina maana kwenu? Maana tanzania ya leo imegeuzwa SHAMBA LA BIBI inatosha sasa kila mtanzania aseme inafu iz inafu mtu akila mali ya umaa tumshuhulikie wenyewe ili kuiweka nchi kwenye msitari unaotakiwa,mjomba usiibanie hii comment yangu coz inaniuma sn sn.

    ReplyDelete
  2. TANZANIA ITAJENGWA NA WATANZANIA WENYEWE.

    WaTAnzania tunatakiwa tuwe wa-bunifu wa kuwabana wabadhilifu wote, kwenye wizara zote za serikali yetu ya TANZANIA.

    mdau holland.

    ReplyDelete
  3. Yes, that is what I know of you. Work, honesty and patriotism.
    God bless you, and all those in accord with the law.
    Regards,
    Thursday Breakfast!

    ReplyDelete
  4. I still don't understand how an employee can draft his/her own KPI, is that not the job of the Minister?

    ReplyDelete
  5. I totally support mdau wa kwanza - the mdudu. Kuongezea, ndugu Nyalandu seems to be the right man for the job- for now. Kwa hiyo namuomba atume jeshi la taifa kwenye mbuga zetu za wanyama kugombana na adui wa Tanzania wanao uwa wanyama wetu waporini. Na hao maprofessa njaa waliotimuliwa - check their ethnicity. They cannot be Tanzanians, can they? Confiscate all their wealth, auction them and finance the troops who should be sent to sort out the poachers who are destroying our wildlife of not just the majestic animals but also our birds, snakes etc. I hope and pray that Ndugu Nyalandu will succeed in getting the right people for the job - people who love and care for TZ. Not corrupt individuals wanao chukua chao mapema-so goes the saying... Mungu Ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  6. Huyu Professor ni kafara

    Usiishie idara ya wanyamapori tu endelea na mamlaka ya misitu kila kukicha miti inakatwa magogo yanaenda lakini uko kimya nako huko ingia

    ReplyDelete
  7. Actions speak louder than words-Safi sana Mh. Waziri

    David V

    ReplyDelete
  8. Tusikilize..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...