Waziri wa Uhamiaji wa Uingereza, Mark Harper (pichani), amejiuzulu baada ya kujulikana kuwa amemuajiri mtu asiyekuwa na kibali cha kubaki nchini.
Alieleza kuwa alidanganywa na mwanamke mmoja aliyemuonesha nyaraka za bandia, alipomuajiri kusafisha nyumba yake.
Bwana Harper alisema kwa sababu alichangia kupitisha bungeni sheria ngumu kuhusu uhamiaji, alihisi inambidi kuwajibika zaidi kushinda wengine.

Chama cha Conservative kimeahidi kupunguza idadi ya watu wanaohamia Uingereza kutoka malaki na kuwa elfu kadha tu.
Chanzo: BBC Swahili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Nimeipenda, no kujishauri mara mia mia linapofika suala la uwajibikaji

    ReplyDelete
  2. Huyu hajafikia hata zile sifa za kuitwa waziri "mzigo" lakini kwa hiari yake kakubali kubwaga manyanga.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...