Waziri wa Uhamiaji wa Uingereza, Mark Harper (pichani), amejiuzulu baada ya kujulikana kuwa amemuajiri mtu asiyekuwa na kibali cha kubaki nchini.
Alieleza kuwa alidanganywa na mwanamke mmoja aliyemuonesha nyaraka za bandia, alipomuajiri kusafisha nyumba yake.
Bwana Harper alisema kwa sababu alichangia kupitisha bungeni sheria ngumu kuhusu uhamiaji, alihisi inambidi kuwajibika zaidi kushinda wengine.
Chama cha Conservative kimeahidi kupunguza idadi ya watu wanaohamia Uingereza kutoka malaki na kuwa elfu kadha tu.
Chanzo: BBC Swahili
Nimeipenda, no kujishauri mara mia mia linapofika suala la uwajibikaji
ReplyDeleteHuyu hajafikia hata zile sifa za kuitwa waziri "mzigo" lakini kwa hiari yake kakubali kubwaga manyanga.
ReplyDelete