Tanzanian nationality law is the law which deals with citizenship and other forms of nationality. A Tanzanian citizen is anyone who is in possession of citizenship to the United Republic of Tanzania. Nationality law is mentioned in the Constitution of Tanzania. 
The citizenship law was first implemented after independence in 1961, and amended in 1964 when Tanganyika and Zanzibar united to form Tanzania. 
For more CLICK HERE

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. Interesting, so a Tanzania woman married to a foreigner in a country where dual citizenship is allowable, can keep her Bongo land citizenship and acquire her adoptive country citizenship, but men can`t do the same.
    Most of the Asians have dual citizenship ages ago.
    Mipingo ndo walala hoi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sexism.... Tanzanian men are being screwed... This should not be a dual citizenship argument but an "equal rights for men" debate...

      Delete
  2. Mambo makuu yajayo mbele yetu:

    1.Tunaelekea kwenye Uchumi wa Gesi na Mafuta ukiambatana na Utajiri mkubwa sana wa Madini kama mnavyoona kufikia Tanzania na Raisi wetu Kikwete wanaonewa wiuvu na majirani zetu EAC, inatengwa na kufanyiwa mipango ya siri.

    2.Tunaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu 2015 huku ''utajiri No.1'' hapo juu ukiwa kibindoni.

    3.Uchumi wa Dunia umeyumba na sasa Mabepari wa ulimwengu wanahamishia kuinusuru Mitaji yao nchi zinazoendelea na zenye mali kama Tanzania.

    4.Katiba mpya inajadiliwa sasa.

    5.Tanzania ili kukabiliana na Ufisadi imepelekea Wakubwa kupendekeza turudi ktk Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea ama kurejesha vionjo vyake vya muhimu kama Azimio la Arusha na Mashariti na Sifa za Uongozi Bora.

    HIVYO NDUGU ZETU MADIASPORA MAJUU KARIBUNI TANZANIA LAKINI MUWE TAYARI KUINGIA KTK SIASA YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA NA KUKUBALI URAIA WA NCHI MOJA KWA KUUKANA URAIA WENU WA MAJUU!!!

    ReplyDelete
  3. Mdau N0#2 naona uliomba visa ya kwenda sehemu ukanyimwa, sasa chuki imekujaa. Piga moyo konde labda siku moja utafanikiwa. Nakumbuka ndugu zako siyo waliokunyima bali kila mtu na bahati yake(au mtoto wa wakubwa,LOL!). Na huo utajiri unaousema wewe hauna tija kwa watu wa chini, kwani tumeona mataifa mengi masikini yaliyojaliwa utajiri umegeuka kuwa laana. Mfano, Nigeria na TZ yenyewe. TZ ina madini muda sana je faida yake iko wapi?! Angalia sehemu za karibu wanapochimba madini, hawana maji, umeme, mashule yaani vitu vya msingi. Sasa na amini kweli siye weusi miili yetu mieusi na roho zetu nyeusi, angalia jamaa wanvyopinga ndugu zao kuwa uraia pacha wakati watu wengine kama wahindi mnasema sawa.

    ReplyDelete
  4. ndio maana wengi wenu mnafeli mitihani yenu. 'wikipedia' sio source ya kuaminika kuanzisha mijadala muhimu kama hii..

    ReplyDelete
  5. Wengi mlio majuu nakupata makaratasi ya huko mliukana uraia wenu wa Tz na wengine kwa utashi wenu ilifika mpaka kuipaka matope Tz ili yenu ya kupata makatarasi yajipe,jee leo zile sababu mlizozidai ovu mnafanyiwa huku mmeziweka wapi. Mjaalie mwenye uraia miwili mwanamichezo mahiri kama Tz itakuwa ipambane na huo uraia wake mwengine jee atachezea wapi.Kama ni mwanajeshiau anazo mbinu za kimapambano kama likitokea la Tz ipambane na nchi hiyo atapambana akiwa na uraia wa wapi. Kiujumla busara kuruhusu kuwa mtu mmoja na Uraia miwili.

    ReplyDelete
  6. Anonymous wa tano, unaweza kuandika kwenye mtandao lakini naona bado huelewi,au inwezekana uanaadika kwa makusudi ili kumpatia Michuzi maoni mengi. Labda, si vyema kutokukujibu inawezekana akili yako ndiyo ilipofikia kiwango. Angalia mataifa mengi ya uraia pacha yanafanyaje kuhusu mchezaji mwenye uraia pacha. Yeye ndiye anachagua taifa ghani achezee na baada ya hapo sheria za FIFA zinafuata. Tanzania inakosa wachezaji wengi wenye utalaamu ambao wana asili ya kitanzania wanaocheza nje'. Kuhusu mwanajeshi Tanzania aina sifa ya kivita kana kwamba wanajeshi wanweza kusaliti taifa moja au lingine. Jamani acheni chuki chuki zisizo kuwa na tija. Na si kweli ya kwamba kila Mtanzania ameikana TZ,wengine tulizaliwa na uaraia wa mataifa mengine. Na kusema kweli uraia wa TZ sio ishu kabisa kwangu. Maisha yamekwenda na yatakwenda. Ndiyo napenda TZ kwa ajili ya ndugu na rafiki, lakini kwa maneno kama haya watu wanaongea humu, sioni faida ya kuwa MTZ. Lakini huku niliko ni faida kimaisha. Wameniwezesha kwenda shule(na sijatumia hela za kodi ya walala hoi kama wengi mnaoandika humu), wamenipa nafasi ya maisha bora kidogo, mfano toka niko sekondali nina gari na si mtoto wa kigogo au tajiri fulani wa bongo. Na hizo rehema za gesi, madini, nakadhalika na uhakika ni sifiri kwangu kwani hazitanifikia bali wakuu. mliowachagua ndiyo watazila.

    ReplyDelete
  7. Watu wengine sijui kwanini wana mawazo ya kizamani ambayo ni zaidi ya vichekesho. Sasa huyu hapa anasema kama una uraia wa nchi mbili utachezea wapi? Ningemwambia utachezea nchi unayoipenda zaidi.....mfano kuna mchezaji wa Ghana anayeitwa Jerome Boateng anyechezea timu ya taifa ya Ujerumani kwa sababu anaipenda ujerumani zaidi, ila kombe hili la dunia linalokuja ataichezea Ghana akiwa na mdogo wake. Kuichezea timu unayoipenda ni mapenzi yako kwa sababu michezo siyo ugomvi na una hiyari. Kuhusu ikitokea vita mwenye uraia wa nchi mbili atapigania upande upi? Jibu ni kuwa siyo lazima apigane au awe askari ila anaweza kuwa balozi mzuri wa kuandamana na kushauri nchi hizo zinazotaka kupigana ziache kupigana kwani kupigana hakuna tija. Watanzania bado tuna mawazo ya kupigana hadi leo? Kwa nini hatuangalii faida zaidi ya hasara za uraia wa nchi mbili? Binafsi naishi Tanzania na sitegemei kuwa na uraia wa nchi nyingine lakini kwa wale walioweza kuwa raia wa nchi nyingine siwaonei wivu. Tunapenda kuona watanzania wa upande mwingine wa dunia wakiwekeza na kutengeneza ajira kwenye nchi yetu tuachane na mambo yaliyopita ya kijamaa kuwa kazi siku zote zinatengenezwa na serikali......Tunawahitaji watu wenye mitaji ili watuajiri, ni fahari kuajiri na mtanzania.

    ReplyDelete
  8. Mdau wa kwanza kaiona shida.... Wanaume hawana ruhusa ya kiwa ya pasi pacha, lakini wanawake wanayo!! Haha, reverse sexism... Wanaume tujitetee haki zetu!!

    ReplyDelete
  9. Kwani tupa uhakika gani kwa huyo mraia pacha na akiwa mchezaji bora kuwa ataichezea Tz.Mdau wa sita umesema "uamuzi achezee wapi ni uamuzi wake". Basi hilo ndilo lenye mushkeli katika katiba tunayotengeneza. Ya nini ambiguities kama hizo. Ona Mfano,mwanariadha Mo Farah mzaliwa wa Somalia na ana medali za dhahabu 6 na silver moja lakini hakuna hata moja iliyopigiwa wimbo wa Somalia. Kisa ndio kwa mabwana zake.Somali imepata nini kuwa na mzaliwa kama yule.Mdau sasa Tz inapapatikiwa.Ina gold,almasi,gesi asilia,petrolium,Tanzanite na hata ile nguvu ya madola makubwa Uranium ndio mana maraisi wa mataifa makubwa hawaondoki Tz .Rome was not built in a day slowly,slowly but steadily,we will win the race . Hatukuhitajini sasa mlo ukana uraia wenu

    ReplyDelete
  10. Ndugu zangu wana Diaspora ,take my advice - stay away from these kinds of discussions.Tujenge hoja zetu at the right places.humu katika blogs hizi mtaishia kutukanana na kukashifiana kwani walio wengi wanaopinga hoja hii ni watu wanaotawaliwa na ulimbukeni,wivu na negativity.

    ReplyDelete
  11. Wewe mdau wa hapo juu unayesema Mo Farah hakuiletea Somalia medali lakini mimi na wewe na wwngine wote duniani tunajua anatoka Somalia....je hiyo siyo sifa ya Somalia? Jamii ya kimataifa imeshajua kuwa kumbe wasomali wanaweza michezo, ni sifa hiyo tayari. Sasa makocha wa mbio wapo wanasaka vipaji huko Somalia. Wewe unafikiri Mo farah angekuwa Somalia angefika wapi....pengine angeshauawa. Waacheni wivu kama nilivyosema mimi sitegemei kuishi nchi nyingine lakini ni muumini mkubwa wa kuona watanzania wakiwa sehemu zote duniani wakichangamkia opportunities ili kuweza kutunza familia zao hapa nyumbani, kwani wakiwa na uraia wao wa kuzaliwa sisi tusio nao tunakosa nini? Bado tuna shida ya ajira hapa nyumbani tunahitaji watanzania waende nje kwa wingi. Hivi hizo nchi nyingine nyingi ikiwamo majirani zetu Kenya na Uganda mbona wanakubali uraia pacha...sisi tuna tatizo gani kwanini tunakuwa wagumu? Au bado tuna mentality za kijamaa?

    ReplyDelete
  12. JAMANI EEE TULIZENI JAZBA!!!
    MIMI NADHANI HAYA MAONI YENU KAMA KAKA ANKEL ATAYAFIKISHA KWA WAHISIKA YATAFANYIWA UCHAMBUZI KISHA YATAPIGIWA KURA NA UKWELI UTAJULIKANA, NITOWE MFANO KIDOGO, YUKO MDAU ALIESEMA MEEEEENGI NA KASHFA KIBAO KWA TZ, HADI ALIDAI KUSEMA HANA HAJA YA HIYO PASS ILIOPINDA, SASA NASEMA HIVIII NDUGU ZANGU MANAO TAKA URAIA PACHA JENGENI HOJA ZA MSINGI NA ZENYE TIJA AMBAZO ZINAWEZA KUWAPA POINT NYINGI KWA HOJA ZA MSINGI MTAKAZO WASILISHA HAPA, SIO MATUSI NA KEJELI KWANI SOTE NI WANA TZ NA TUNAJUWA KUWA HIYO GESI, MADINI, MBUGA, BANDARI HAVIMFIKIII MLALA HOI NA WACHANGIAJI WENGI NDIO HAO WANAO KIMBILIA KWENYE UTAJIRI WA VIONGOZI BADALA YA KUANGALIA UHALALI WA MTU KWAO. IKO SIKU HAKI ZA BINAADAMU ZITAINGILIA KATI NA HAKI ITATENDKA BILA PANGA WALA KIBOKO.(TOWENI COMMENTS ZENYE TIJA HASWA KWA NYIE MLIOKO NJE) SISI WA NDANI TUECHENI TUWABEZE MAAANA HAKUNA ATAKAE TUJADILI KWANI HATUHITAJI KUTOKA NJE YA TZ.

    ReplyDelete
  13. Wabongo wasiku hizi wengi roho mbaya.Kwa mtu ambaye hahitaji uraia wa zaidi ya nchi moja hana sababu kumzuia mwenye kuhitaji uraia huo. Ifike mahali tukubaliane kuwa wenye uraia upi wana haki zipi na wajibu upi kwani tunajua huwezi kula kwenu A kisha uje na kwenu B nako ukala. Mimi kimsingi nahitaji uraia wa nchi nne. Ninayo maelezo kwanini nahitaji.

    ReplyDelete
  14. diaspora mnaweza kusaidia iliokua nchi yenu na watu wake hata mkiwa na nyiraia(wingi wa uraia) za kigeni.

    ReplyDelete
  15. Mdau wa 14 unaohitaji Uraia wa nchi 4 hapo juu.


    ......Wabongo wasiku hizi wengi roho mbaya.Kwa mtu ambaye hahitaji uraia wa zaidi ya nchi moja hana sababu kumzuia mwenye kuhitaji uraia huo. Ifike mahali tukubaliane kuwa wenye uraia upi wana haki zipi na wajibu upi kwani tunajua huwezi kula kwenu A kisha uje na kwenu B nako ukala. Mimi kimsingi nahitaji uraia wa nchi nne. Ninayo maelezo kwanini nahitaji........

    1.SASA URAIA WA NCHI ZOTE 4 ILI IWEJE?

    2.HUELEWI ILE TU KITENDO CHA KUUKANA URAIA WAKO WA TANZANIA HAPO KABLA NI DHAMBI KUBWA SANA?

    3.ULIONA WAPI NYOKA AKAWA NA VICHWA VINNE?,,,LABDA AWE NI NYOKA JINI!

    4.AU UNATAKA KUTULETEA ZA KICHINA CHINA ZA SIMU ZENYE LAINI 4 AMBAPO MTU MMOJA AKIZIMILIKI ZOTE AKIPIGIWA KWA WAKATI MMOJA ATAPOKEA IPI NA ATAACHA IPI?,,,SIMU ZA LAINI 4 ALIZOTULETEA MCHINA NI MOJA YA UTAAHIRA ALITULETEA MCHINA KULINGANA NA UJINGA WETU WATU WANAZIMILIKI BILA KUJUA MAANA YAKE NI KWA NINI?,,,NI KUWA ILI WATU WAWE MAZEZETA KUTUMIA MUDA MWINGI KTK MAONGEZI YA SIMU BADALA YA KUFANYA KAZI !

    5.HALAFU NDIO WEWE WEWE TENA ULIYE UASI UTANZANIA KWA KUKANA URAIA NA KUKEJELI NCHI NA KUIPAKAZIA VIBAYA HUKO NJE UNATAKA UREJESHEWE URAIA NA IKIWEZEKANA UWE KIONGOZI WA TANZANIA TENA!

    ReplyDelete
  16. Mdau wa 14 tutawaheshimu Madiaspora ambao hawakuukana Uraia wa Tanzania TUNAWAONA HATA KTK VIKAO VYA VYAMA VYOTE VYA SIASA ktk CCM na Chadema lakini hatukubaliani na WALIOKANA URAIA WA TANZANIA!

    WALIOKANA URAIA WA TANZANIA WAENDELEE KUBEBA MABOKSI MAJUU.

    ReplyDelete
  17. WENGI HAPA HAWACHANGII KWA KUFUATA UZITO WA MADA, SIDHANI KAMA KUNAYEYOTE AMBAE AMEGUSIA KUJA KULA WALA KULALA LAAAHASHA, BALI WENZETU HUKO NJE WANATAKA KUTAMBULIWA RASMI KAMA RAIA WENGINE NA KUWA NA HAKI KAMILI SIO KUWAAMBIA ETI WAMEKANA UTZ. Hawatakiwi kulipa visa, wanahaki ya kujenga na kuwekeza kama wamiliki halali, na haki ya kupiga kura wakati wa chaguzi zetu, Maana yupo mdada wa USA nilimsikia akisema eti huruhusiwi kujenga kama huna una uraia ya kigeni na hali wewe umeondoka ukiwa na shamba lako mazao eti leo unataka kuliendeleza serikali inasema huna haki sidhani kama ni kweli na kama hali ndio iko hivyo basi wanaotaka mabadiliko ya hii sheria wanahaki, kwani tunaona hapa TZ wageni ambao hawakuzaliwa wala hawakuwahi kuja na chochote wamejenga majumba ya kifahari kwa kuwa tu anajuwana na mkubwa fulani. Jamani wa TZ tubadilike kwani hatuwezi kuishi chini ya majina ya wakuu wa nchi au Vigogo kama mnavyo waita. Ifike wakati DEMOCRASY inatumika kama ilivyo kwa kila mtanzania. Kwahiyo watanzania waishio nje siokwamba wanataka GESI NA MAFUTA AU DHAHABU NA ALMASI bali wanataka haki ya kutambuliwa kama watanzania wengine, tene niseme kuwa tuache tabia ya kusema eti WAMEUKANA U TZ hako hivyo, kwani waliozaliwa nao wasemeje????

    ReplyDelete
  18. Hahahaaa,wenzetu wa ughaibuni.Jisikieni raha kuwa mko ugenini,na ya huku tuwachieni wenyewe.Bado mna haki fulani ziendelezeni haki hizo.Mna haki za kusaidia mkipenda,lakini haki ya kuja kupiga kura kwa ajili ya kuchagua au kuchaguliwa hiyo haki mliikataa pale mlipoukana uraia wa Tanzania. Haki ya kuja na kununua mapori ya ardhi mkayamiliki chini ya kivuli Raia haikubaliki.Hapa ingieni kwa viza,mkilipia viza au exit viza tunazihitaji fedha kama hizo .Ni mara ngapi kwani viongozi wa juu kama maraisi wamekuja huko na kukushaurini muwekeze huku jee ni wangapi walioitikia wito kama huo.Sekta ya kilimo inahitaji mapinduzi ya kilimo agrarian revolution jee wangapi waliojitokeza kiipa msukumo.Sekta ya uvuvi inahitaji kupewa kipa umbele na nyinyi mnalijuwa hilo,jee wangapi mmeonesha kusaidia,secta ya viwanda ndio hivyo hivyo yataka msukumo jee mmezisaidia? Au mwataka uraia pacha kama ni shoo tu kuja kuwakoga wazalendo wa kweli.Endeleeni kununua viza kuingia Bongo. You deserve to taste the burden of your sins.Unaukana uraia wako ??

    ReplyDelete
    Replies
    1. You are not very intelligent... If I tell you that you have and have had female MPs with dual nationality what will you say?... Na sheria za Leo hazizuii kuwa Na waziri wa like mwenye pasi pacha...

      Delete
  19. HALLO JAMANI MLIOKUWA NA URAIA WA NCHI ZINGINE MUENDELEE TU HIVYO HIVYO, MSITULETEE MIZENGWE TUNA MENGI YA KUTATUA SIO NA LENU TENA LA URAIA WA NCHI MBILI KAMA SIMU ZA KICHINA.

    SASA MILUTAKIA NINI HUO URAIA WAHUKO NA KUUKANA VIKALI UTANZANIA MLIKUBALIWA BILA MATATIZO WALA KULAZIMISHWA SASA LEO IMEKUWA VIPI TENA?

    TUACHENI TANZANIA INA MAMBO MENGI YA KATATUA EMBU TUPENI TIME OUT ILI TU CONCETRATE NA CCM, NA CHADEMA . SUBIRINI BAADA YA UCHAGUZI 2015 NDIO MUSNZISHE ISSUE HIO YA URAIA , PLEASE

    ReplyDelete
  20. Ndio maana Wanaume Tanzania tumelala mpaka Leo... Kelele kibao kuhusu pasi pacha nk.... Wenye akili juu (Anon no 1)ameisha soma kwamba Tanzania chini ya Mwalimu ilikua Na wabunge wa kike wenye pasi za nje!! Kelele kibao huku haki za wanaume ndio hazipatikani...

    ReplyDelete
  21. Mwaka 1970 baada ya kufuzu Mlimani, tuliposomeshwa kwa pesa za serikali, ilijafahamika kuwa wasichana kama wanne hivi wa Kitanzania waliolewa nna na raia wa nchi zanje na kupelekwa huko kwa waume zao. Tulikuwa tuifanyie kazi nchi yetu kwa miaka mitatu bila kujiuzulu ili kifidia gharama ya usomi.Tulitii; lakini hao wasichana waliruka bila adhabu yeyote.


    Tuliokuwa tunafanya kazi Moshi mjini, tulimtaka Mbunge Leons Ngalai wa Moshi atutafutie sababu yake. Aliambiwa na serikali kuwa wasichana hawakuwa na kizuizi cha kuolewa nje. Hivyo, ilikuwa na maana kwa nini na sisi wavulana tulioe wasichana wa nchi za nje!

    ReplyDelete
  22. Nyie watu acha roho mbaya.Nchi hii ni kubwa sana.Kama mtoto mpotevu anataka kurejea,aachwe aje.Tujenge taifa letu kongwe!Hizi phobia juu ya wenzetu walioko Ughaibuni hazina tija wala maana yoyote.Mfano ni wenzetu walokimbia siasa kali za Visiwani Enzi zile za kuoa vimwana weupe.Leo ni wasomi na wana mali;acha waje tu!

    ReplyDelete
  23. Hatuwezi kuwapa Uraia mara ya pili watu WASALITI WA TANZANIA !

    USALITI WA KUUKANA URAIA ama KUUPOTEZA mmbaya heri yam Mchawi kuliko Msaliti.

    Kwanza wengi mmeishi nje ya nchi na kufanya shughuli chafu za Uhalifu huku mkiishi nje ya Sheria!

    Leo baada ya kuinyea sana Tanzania na kuichafua sana huko nje ya nchi sasa mnataka mrudi tena hapa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...