Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko Rashid Salum Ali wa kwanza (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ wa kwanza (kulia) wakitia saini makubaliano ya ubadilishanaji majengo ya Taasisi hizo mbili katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Benki ya Kiislamu ya PBZ Mpirani mjni Zanzibar. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya PBZ Abrahamani Mwinyi.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko Rashid Salum Ali wa kwanza (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ wa kwanza (kulia) wakibadilishana hati ya makubaliano ya ubadilishanaji majengo ya Taasisi hizo mbili ambapo PBZ itachukua jingo la Ofisi ya Biashara ya Magari liliopo Malindi na Wizara ya Biashara itachukua Jengo la Makao Makuu ya sasa ya PBZ la Darajani.
Baadhi ya Maofisa wa PBZ wakiangalia utiaji saini wa makubaliano ya ubadilishanaji wa majengo ya Benki hiyo na iliyokuwa Ofisi ya Shirika la Biashara ya Magari lililochini ya Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko.
Picha ya pamoja ya maafisa wa PBZ na Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko baada ya kumalizika hafla ya makubaliano ya ubadilishanaji wa majengo ya Taasisi hzo mbili iliyofanyika Makao Makuu ya Benki ya kiislamu ya PBZ Mpirani mjini Zanzibar. Picha no.05- Jengo la Ofisi ya Biashara ya Magari liliopo Malindi Mjini Zanzibar ambalo limekabidhiwa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kwa ajili ya kujenga Makao Makuu Mapya ya Benki hiyo.
Jengo la Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) liliopo Darajani Mjini Zanzibar ambalo limekabidhiwa Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko. (Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. PBZ mjenge jengo lenu sasa kila siku mnahamia katika majengo ya watu wengine tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...