Na Boniface Wambura, Dar es Salaam
MECHI za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zilizohusisha timu za Yanga na Simba, na kuchezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki zimeingiza jumla ya sh. 101,165,000.
Yanga ambayo iibugiza Ruvu Shooting mabao 7-0 mechi yake iliingiza sh. 68,450,000 kutokana na washabiki 11,972 kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.
Katika mechi hiyo kila klabu ilipata mgao wa sh. 15,687,488 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa kutokana na mapato hayo ni sh. 10,441,525.42. Gharama za tiketi ni sh. 3,813,600 na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ilipata sh. 4,877,538.71. Uwanja sh. 8,129,231.19.

Mrisho Ngassa kushoto na Emmanuel Okwi kulia waling'ara wakati Yanga ikiishinda  Ruvu Shooting Stars bao 7-0 Jumamosi


Gharama za mchezo zilikuwa sh. 4,877,538.71 wakati Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,438,769.36. Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) kila kimoja kilipata sh. 945,110.
Nayo mechi ya Simba na JKT Ruvu ilishuhudia na watazamaji 5,850 na kuingiza sh. 32,715,00 kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. 
Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 4,990,423.73.
Kila klabu ilipata mgawo wa sh. 7,428,742 wakati tiketi ni sh. 2,542,400 huku gharama za mechi zikiwa 2,266,395.86. 
Uwanja ulipata sh. 3,777,326.44 wakati Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ni sh. 2,266,395.86.
Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) ulipata mgawo wa sh. 1,133,167.93 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 881,376.17.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...