Ofisa Uhusiano na Matukio wa Airtel Tanzania, Dangio Kaniki (kulia)akiteta na Afisa Mnadhimu wa Polisi Kinondoni, Bibie Juma Athumani (wa kwanza kushoto)baada ya Airtel kukabidhi viti na meza kwa ajili ya polisi wa kituo cha oysterbay hivi karibuni.Wanaoshuhudia ni baadhi ya maofisa wa Polisi wa kituo hicho.
Ofisa Uhusiano na Matukio wa Airtel Tanzania, Dangio Kaniki (kulia) akisalimiana na Afisa Mnadhimu wa Polisi Kinondoni, Bibie Juma Athumani baada ya Airtel kukabidhi viti na meza kwa ajili ya polisi wa kituo cha oysterbay hivi karibuni.Wanaoshuhudia ni baadhi ya maofisa wa kituo hicho.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imeendelea kuunga mkono serikali kupitia jeshi la polisi usalama barabarani kwa kuwapatia vifaa vya ofisi kwa ajili ya kituo cha Usalama Barabarani cha Oysterbay kilichopo wilaya ya Kinondoni.
  
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Afisa uhusiano na matukio wa Airtel  Dangio Kaniki alisema “Airtel inatambua umuhimu wa kazi inayofanywa na Kitengo cha Usalama Barabarani katika kusimamia na kuhakikisha usalama wa watanzania na kuamua kushirikina nao katika kuboresha mazingira ya kufanyia kazi. Leo tunatoa meza pamoja viti vya ofisi kwa kitu hiki cha polisi oystebay tukiamini   kwamba tutaongeza ari na moyo wa kujituma kwa maofisa hawa  na kuleta ufanisi wa kazi ,”

kwa miaka mitano mfululizo sasa Airtel imekuwa ikishirikiana na jeshi la polisi katika kufanikisha zoezi la usalama barabarani hivyo tumeonelea ni vyema kuendelea kushirikiana nao  ili kuleta mafanikio makubwa katika kutekeleza kazi zao  nchini.

Airtel itaendelea na dhamira yake  yakushirikiana na jeshi la polisi katika juhudi za kuhakikisha usalama barabarani unazingatiwa na kuhakikisha ajali za barabarani zinapungua kwa kiasi kikubwa nchini

Kwa upande wake, Afisa Mnadhimu wa Polisi  Kinondoni, SSP. Bibie Juma Athuman alisema “Naishukuru sana Airtel kwa kutoa mchango wa vifaa vya ofisi kwenye kituo changu kwani tulikuwa na uhaba mkubwa wa viti na meza za kukalia wafanyakazi pindi wakiwapo ofisini. Msaada huu utasaidia kutatua matatizo tuliyokuwa nayo na kuboresha mazingira ya wafanyakazi wa kituo hiki kuwa mazuri zaidi.  Tunawaomba makampuni mengine pia yashiriki katika kuwawezesha jeshi la polisi na kuchangia katika kuhakikisha usalama barabarani unazingatiwa kama wanavyofanya wenzetu wa Airtel.”

 Msaada huo ni muendelezo wa mpango wa Airtel kusaidia Polisi  Usalama Barabarani hapa nchini ambapo mwezi Septemba mwaka jana kampuni hiyo imetoa T-shirt zenye ujumbe Maalum wa Usalama Barabarani, stika zenye ujumbe wa kuelimisha na mafunzo kwa ajili ya kuelimisha Usalama Barabarani kwa waendesha bodaboda mkoani Mwanza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...