Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga akifungua mkutano ulijadili namna bora ya kuwahusisha wadau wa Sekta ya Lishe katika Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini na zinazoishi katika mazingira hatarishi, (PSSN) unaoratibiwa na TASAF
Mkurugenzi wa uratibu wa Shughuli za Serikali katika Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Obeyi Assery akizungumza na washiriki wa mkutano (hawapo pichani) uliojadili namna ya kuhusisha masuala ya lishe katika Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa CEEMI Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Lishe katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk Vicent Assey akizungumza na wataalam walioshiriki katika mkutano uliojadili namna ya kuhusisha masuala ya lishe katika mpango wa kunusuru kaya masikini na zinazoishi katika mazingira hatarishi unaoratibiwa na TASAF
 Baadhi ya washiriki wa mkutano uliondaliwa na TASAF kujadili namna bora ya kuhusisha masuala ya lishe katika mpango wa kunusuru kaya masikini sana nchini wakimsikiliza mkurugenzi Mtendaji wa TASAF , Ladislaus Mwamanga ( hayupo pichani) wakati alipofungua mkutano huo kwenye ukumbi wa CEEM ,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ladislaus Mwamanga (wapili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano uliojadili namna ya kuhusisha masuala ya lishe katika mpango wa kunusuru kaya masikini sana na zinazoishi katika mazingira hatarishi uliofanyika katika ukumbi wa CEEMI jijini Dar es Salaam
===========  ===========   ============
TASAF NA MKAKATI WA KUKABILIANA NA TATIZO LA LISHE DUNI NCHINI.


Mfuko wa Maendeleo ya Jamii nchini TASAF kupitia Mpango wa kunusuru kaya masikini sana na zilizo katika mazingira hatarishi ,PSSN umekutana na wadau wa sekta mbalimbali za kiserikali kujadili namna ya kushirikiana katika kuhakikisha kuwa suala la lishe bora linapewa umuhimu mkubwa ili kupambana na tatizo la utapiamlo hususani kwa watoto nchini.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa wadau wa sekta za afya na lishe kwenye ukumbi wa CEEMI jijini DSM,Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Ladislaus Mwamanga amesema jitihada zaidi zinapaswa kuelekezwa katika kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kuboresha afya kwa kutumia lishe bora hususani kwa watoto ili kujenga makuzi sahihi ya ubongo wao.

Mwamanga amesema TASAF kwa upande wake imeweka mfumo imara wa kuwahusisha watalaamu wake ambao wamesambazwa katika maeneo mbalimbali nchini kote na kutoa rai ya kuwahusisha katika kampeni mbalimbali za kuwaelimisha wananchi juu  ya matumizi sahihi ya vyakula kwenye maeneo husika.

Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF amesisitza kuwa pamoja na TASAF kuanza utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya masikini na zinazoishi katika mazingira hatarishi ambapo suala la lishe ni moja ya vipengele muhimu, ni vema sekta nyingine pia zikashirikiana na taasisi yake katika kuhakikisha kuwa wananchi wanapata elimu sahihi juu ya namna bora ya kuboresha lishe hususani kwa watoto na akinamama wajawazito.

Mwamanga pia ametoa rai kwa wataalam kutumia mbinu mbalimbali za kuwasilisha ujumbe sahihi wa masuala ya lishe na kuzisambaza kwa walengwa jambo litakalosaidia kupambana na tatizo la kudumaa kwa makuzi na ubongo kwa watoto ambapo kwa sasa inakadiriwa kuwa asilimia 42 ya watoto nchini wamedumaa kimakuzi.

Mapema akizungumza katika mkutano huo ulioshirikisha wadau kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Wizara ya mifugo na Uvuvi ,Wizara ya Kilimo,Taasisi ya Lishe na Chakula na wataalamu kutoka TASAF,Mkurugenzi wa uratibu wa Shughuli za Serikali katika Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Obeyi Assery amesema suala la kudumaa katika makuzi ya mtoto ni tatizo kubwa nchini ambalo linapaswa kutatuliwa kwa nguvu za wadau mbalimbali .

Naye mkurugenzi msaidizi Huduma za Lishe katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk Vicent Assey amepongeza jitihada za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii nchini TASAF kwa kubuni mpango wa kunusuru kaya masikini na zinazoishi kwenye mazingira hatarishi ambapo suala la lishe litawekewa msukumu mkubwa kama moja ya vigezo vya kuzisaidia kaya zitakazoingizwa kwenye mpango huo mkubwa wa aina yake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...