Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao
lililofungwa na Didier Kavumbagu (wa pili kulia), wakati wa mchezo wa Ligi Kuu
ya soka Tanzania Bara ilipopambana na Azam
FC kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. Timu hizo zilitoka
sare ya 1-1.
Heka heka: Golikipa wa timu ya Azam FC, Aishi Salum akiokoa moja ya hatari langoni mwake.
Mfungaji wa bao la Yanga, Didier Kavumbagu akitafuta mbinu za kuwatoka mabeki wa Azam FC.
Beki wa Azam FC, Gadiel Michael akimiliki mpira (kushoto) akiwania mpira huo ni mshambuliaji wa yanga, Hamis Kiiza.
Mashabiki wa Yanga, wakishuhudia pambano hilo.
Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva akimtoka beki wa Azam FC, Bolou Michael. Picha na Francis Dande
Hapa timu ya Wananchi haitapata faini ya TFF au faini ni kwa timu ya Msimbazi?
ReplyDeleteMdau
Mtaa wa Msimbazi