Na Othman Khamis Ame, OMPR
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amefanya ziara fupi ya kukagua ujenzi wa Hoteli Mpya ya Daraja la Saba ya Grand Hayatt inayojengwa katika eneo lililokuwa Starehe Club ndani ya Mji Mkongwe wa Zanzibar.
Ujenzi wa Hoteli hilo inayomilikiwa na Kampuni ya Kimataifa ya ASB Holding’s unafanywa na Kampuni ya Kimataifa ya Ujenzi kutoka Jamuhuri ya Watu wa China ya CRJ.
Kampuni hiyo ya ASB Holding’s katika ujenzi wake huo imechukuwa hatua za matakwa ya Umoja wa Mataifa kupitia Shirika lake la Elimu, Sayansi na Utamaduni { UNESCO } juu ya kuendeleza hifadhi ya Mji Mkongwe wa Zanzibar ambao umo katika makubaliano ya Hifadhi ya Kimataifa.
Ujenzi wa ukuta Maalum wa mita tatu kama yalivyo majengo mengine ya Mji Mkongwe yaliyo pembezoni mwa Bahari unazingatiwa kwenye Hoteli hiyo ili kunusuru athari yoyote ya Maji, Mazingira au matukio ya Dhoruba yanapotokea wakati wowote.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Mji Mkongwe wa Zanzibar Issa Sarboko Makarani alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwamba jengo lililokuwa Mambo Msiige ambalo limeambatana na ujenzi huo linafanyiwa matengenezo makubwa kwa kutumia chokaa ili kulinda uasili wake.
Nd. Sarboko alisema matumizi ya saruji katika majengo ya asili ndani ya Mji Mkongwe yaliyojengwa kwa chokaa na udongo mbali ya kuharibu mfumo wake wa kihistoria lakini pia unaondosha ubadhubuti wa majengo hayo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliupongeza uongozi wa Hoteli hiyo kwa juhudi zake za kuwekeza kitega uchumi kitakachosaidia kunyanyua sekta ya Utalii ambayo hivi sasa imepewa kipaumbele na Serikali.
Uongozi wa Hoteli hiyo ulimuhakikishia Balozi Seif kwamba ujenzi wa mradi huo unatarajiwa kukamilika rasmi mwezi Agosti mwaka huu na ulilazimika kuchelewa kutokana na baadhi ya vifaa vingi vya ujenzi wake kuchelewa kufika Nchini kwa wakati uliopangwa.
Jengo la Hoteli hiyo ya Daraja la Saba litakalokuwa na ghorofa Tatu unatarajiwa kutoa ajira za wafanyakazi wazalendo kati ya sitini na mia moja wakati litakapoanza kutoa huduma zake.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mji Mkongwe wa Zanzibar Nd. Issa Sarboko Makarani akimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Juhudi zilizochukuliwa na Kampuni ya ASB Holdings za ujenzi wa Hoteli ya Daraja la Saba Shangani uliozingatia mpango wa Umoja wa Mtaifa ya Uhifadhi wa Mji Mkongwe. Kulia ya Balozi ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Makazi, Maji na Nishati Nd. Ali Khalil Mirza.
![]() |
Balozi Seif akiangalia mandhari nzuri wa Bahari ya Hindi akiwa juu ya Hoteli ya Daraja la Saba iliyopo Shangani Mjini Zanzibar wakati alipokuwa akikagua maendeleo ya ujenzi wa Hoteli hiyo. |
Moja kati ya vyumba vilivyomo ndani ya Hoteli ya Daraja la Saba iliyopo Shangani Mjini Zanzibar ambayo inaendelea na ujenzi wake ikiwa katika hatua za mwisho mwisho. Picha na Hassan Issa wa OMPR, ZNZ.
Jamani nipelekeni shule: hivi daraja la saba ndio SEVEN STARS? Mbona haielekei kuwa na nyota hizo? Blackmpingo
ReplyDelete