Watoto wenye ulemavu wa kituo cha House of Hope kilichopo mkoani Moshi wamepokea msaada wa fedha zitakazo wawezesha kununua viti maalum vya kutembelea vyenye thamani ya shilingi milioni 5 zilizotolewa na kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania kwa kituo hicho kilichopo chini ya Hospitali ya CCBRT.
Akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kaskazini, Philemon Chacha amesema viti hivyo maalum vya kutembelea vimetolewa kwaajili ya kuwasaidia watoto wenye ulemavu walioko kituoni hapo ambao wamekuwa wakikabiliwa na adha ya kukosa vifaa maalum vitakavyo wawezesha kufanya shughuli zao za kawaidi na hata kujiendeleza kielimu.
“Jamii lazima itambue kwamba walemavu ni watu wakawaida kama walivyo watu wengine, hakuna aliyependa kuwa na maradhi ya namna hiyo isipokuwa ni sehemu tu ya maisha ambayo inaweza ikamkuta kila mmoja. Hivyo ni lazima tuwaangalie na kuwasaidia kwa namna ya kipekee ili nao waweze kujiendeleza na kuishi kama binadamu wengine wa kawaidia” Alisema Chacha na kuongeza.
“Tumeanza na viti hivi tukiamini kuwa vitawawezesha watoto hawa kutoka sehemu moja kwenda nyingine na hata kuwasaidia wale watakao kuwa wanasoma na kufanya shughuli zao za kawaida” alisema Chacha.
Meneja huyo wa Vodacom aliongeza kuwa wamekuwa na Ushirikiano mzuri na Hospitali ya CCBRT katika kutekeleza masuala mbalimbali na kuzisaidia jamii ya Watanzania ikiwa ni pamoja na mradi wa kuwasaidia watu wenye Fistula kupata matibabu bure pamoja na kujenga wadi maalum ya wagonjwa wenye Fistula.
Kwa upande wake Kaimu Meneja wa CCBRT Moshi, Bw. Sabas Kimario kuwa wamekuwa wakishirikiana na kampuni ya Vodacom kupitia taasisi yake ya Vodacom Foundation na wanaendelea kuwashukuru kwa moyo wao wanaouonyesha kwa jamii kwani wengi wanaonekana wamewasahau kabisa watoto wenye ulemavu lakini wao wameliona kuwa hili ni tatizo na kuonyesha jitihada za kuwanusuru watoto hao huku akitanabaisha changamoto mbalimbali zinazowakabili.
“Tumekuwa tukilea watoto hawa wenye Ulemavu katika vituo vyetu kazi ambayo kwa kiasi kikubwa hospitali yetu inajitolea, wakati mwingine gharama inakuwa kubwa na inakuwa vigumu kukidhi mahitaji wa watoto wote tunao walea, misaada ya aina hii inatuwezesha kupunguza changamoto zinazo tukabili,” alisema Kimario.
Amesema hospitali yay a CCBRT inavituo kwa ajili ya kulelea watoto wenye ulemavu na pia wanao wataalamu ambao huwa wanatembelea sehemu mbalimbali hasa maeneo ya vijijini ili kufuatilia maendeleo ya watoto ambao wako chini ya uangalizi wa kituo hicho na kutoa elimu kwa wazazi wao namna ya kukaa na kuwatunza watoto wenye ulemavu ikiwemo namna ya kuwalisha na kuwafanyisha mazoezi.
“Ni furaha kwetu kuona kazi ya kuwatunza na kuwatibu watoto hawa inapothaminiwa na kuongezewa nguvu na wadau wengine kama Vodacom ambao kwa kiasi kikubwa tumekuwa tukishirikiana nao kila siku na ninatoa wito kwa wadau wengine kuendelea kujitokeza na kuwasaidia watoto hawa”, alihitimisha Kimario.
Kwa Upande wao wazazi wenye watoto hao wameishukuru Hospitali ya CCBRT kwa kuendelea kutoa huduma kwa jamii ya Watanzania kwa usawa na kuwa msaada mkubwa hata kwa wale wasiojiweza, Huku wakiishukuru kampuni yaa Vodacom kwa namna ambavyo imeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kutoa misaada ya kujamii, na kuwaomba kuendelea na mchango huo.
“Tunawashukuru wote kwa pamoja kwa namna ambavyo mmeweza kushirikiana na kutoa msaada huu kwa watoto wetu tumefarijika sana na tunaamini mtaendelea kuwakumbuka na wengine wasio na uwezo, ili kuwafanya nao wajisikie ni sehemu ya jamii ya Watanzania, alisema Bi Haika Moja ya Wazazi ya Watoto hao waliopokea msaada huo.
Mtoto Innocent David Mwenye Ulemavu akiwa pamoja na Wazazi wake katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu cha House of Hope kilicho chini ya (CCBRT) kilichopo kata ya kaloleni Manipaa ya Moshi wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa hundi ya SH milioni 5 zilizo tolewa na kampuni ya simu ya mkononi ya Vodacom kwa ajili ya kununua viti maalum 16 vya kutembelea watoto wenye ulemavu.
Baadhi ya wazazi, wafanyakazi wa CCBRT Moshi, na Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom, wakiwa wanasikiliza mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wazazi wa watoto wenye ulemavu wanaolelewa katika kituo cha House of Hope Mkoani Moshi.
Meneja Biashara wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania Lillian Kisamba ( kulia) akimkabidhi Kaimu Meneja wa kituo cha CCBRT Moshi Sabas Kimario( kushoto) Mfano wa hundi ya Sh milioni 5 kwajiri ya kununulia viti maalum kumi na sita (16) vya kutembeleakwa kwa watoto wenye Ulemavu wananaolelewa katika kituo hicho.
Wafanyakazi wa kituo cha (CCBRT) cha mjini Moshi na wafanyakazi wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja punde baada ya kampuni hiyo kufanya makabidhiano ya hundi ya Tsh. Milioni 5 msaada huo ni kwaajiri ya kununulia viti mwendo kwa wenye ulemavu waliopo katika kituo hicho.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...