Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akifungua mkutano wa 58 wa Kamisheni kuhusu Hali ya Wanawake ( CSW) Mkutano huu wa wiki mbili unafanyika hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, na unawakutanisha wanawake wa kada mbalimbali kutoka Serikali Kuu na Asasa za Kiraia. Akifungua mkutano, Katibu Mkuu, pamoja na mambo mengine amewataka wanawake kuendelea kutetea fursa za kijinsia, kupinga ubaguzi wa aina zote na kuhakikisha kwamba sauti ya wanawake na watoto wa kike inaendele kusikika katika ajenda mpya za maendeleo baada ya 2015. Kulia kwake ni Muwakilishi wa Kudumu wa Ufilipino katika Umoja wa Mataifa, Balozi Libran Cabactulan ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mkutano .
Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huu, unawahusisha washiriki kutoka pande zote za Muungano, Tanzania Bara na Visiwani. Pichani ni Bi. Asha Ali Abdulla, Katibu Mkuu, Wizara ya Uwezeshaji, Maendeleo ya Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Tuvako Manongi, Muwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Mhe. Jaji Imani Daud Aboud kutoka Mahakama ya Rufaa ya Tanzania, na Bi. Joyce Mlowe, kutoka Wizara ya Katiba na Sheria wakifuatilia hotuba ya ufunguzi.
Sehemu ya Ujumbe wa Tanzania kutoka kulia Bi. Halima Abdulrahman Omar, Mtaalamu wa Masuala ya Jinsia, Wizara ya Uwezeshaji, Maendeleo ya Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto- Zanzibar, Bi Mhaza Gharib Juma, Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti, Wizara ya Uwezeshaji, Maendeleo ya Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto- Zanzibar, na Bi. Ellen Maduhu, Afisa wa Uwakilishi wa Kudumu anayeshughulikia Kamati ya Tatu ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa inayohusika na Masuala ya Maendeleo ya Jamii na Haki za Binadamu.
Na Mwandishi Maalum
Ikiwa imebakia miezi michache kufikia kilele cha utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Millennia ( MDGs), Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon amewataka wanawake kuendelea kupigania haki zao pamoja na za mtoto wa kike.
Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa, ametoa wito huo siku ya jumatatu, mbele ya mamia ya wanawake kutoka mataifa mbalimbali duniani kote ambao wapo hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kuhudhuria mkutano wa 58 wa Kamisheni kuhusu Hali ya Wanawake ( CSW).
Tanzania inawakilishwa katika mkutano huu ambao ni wa wiki mbili na wajumbe kutoka pande zote za Muungano – Tanzania Bara na Tanzania Visiwani.
Hongera na pongezi za dhati Bi Ellen Maduhu kwa juhudi na utekelezi wa majukumu yako ya kazi. Nakutakia kila la kheri na mafanikio mema katika suala zima la uwajibikaji. Hakika kila penye nia, pana njia, am so proud of you.
ReplyDelete(Classmate)