Kampuni ya Strabag International GmbH inayotekeleza ujenzi wa barabara ya Morogoro kuanzia Kimara hadi Kivukoni  jijini Dar es Salaam imetakiwa kuhakikisha kuwa inakamilisha ujenzi wa sehemu hiyo ndani ya kipindi cha miezi sita ijayo kama mkataba wao unavyoelekeza. 
 Waziri wa Ujenzi Mhe. Magufuli alitoa agizo hilo wakati akiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa barabara kwa ajili ya mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam (Dar es Salaam Bus Rapid Transit - BRT) ambao umeelezewa kuwa na changamoto nyingi kiasi cha kusababisha usumbufu kwa watumia barabara hiyo kwa kipindi kirefu. 
 Akimpatia taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Mtendaji Mkuu wa Tanroads Mhandisi Patrick Mfugale alimjulisha Waziri Magufuli kuwa kwa hivi sasa changamoto nyingi zimefanyiwakazi na mradi unaendelea kusimamiwa kwa karibu ili kuhakikisha kuwa hukuna ucheleweshaji zaidi katika hatua hii iliyobaki. 
 Mkataba wa ujenzi wa barabara hizi pamoja na vituo vya mabasi ulisainiwa mwezi Desemba mwaka 2012 ukiwa umepangwa kukamilika katika kipindi cha miaka mitatu kwa gharama ya Shilingi bilioni 280.
Sehemu ya Magomeni jijini Dar es salaam ikonesha maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo
Kituo cha Magomeni Kagera
Daraja la Manzese pamebadilika
Daraja la waendao kwa miguu stendi ya mabasi ya bara ya Ubungo
Flyover ya waendao kwa miguu Ubungo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. SAFI SANA. MRADI HUU UTABADILISHA MAISHA YA WENGI. LAKINI KUNA KITU SIJAELEWA. NI KWA NINI BARABARA YA JUU PALE UBUNGO ISIUNGANISHWE KWENYE HUU MRADI? HII NI ISHARA KUWA UJENZI WA FLYOVER HII NI BADO SANA. KAMA UKO KARIBU BASI WANASUBIRI KUBOMOA BARABARA MPYA KAMA ILIVYO DESTURI.

    ReplyDelete
  2. Michu tafadhari mara kadhaa nimejitahidi kupiga debe kuhusu miundombinu kuwa user-friendly kwa walemavu wazee na wenye watoto ikijumuisha mabasi.peleka hii ms kwa wahusika tafadhari .

    ReplyDelete
  3. The mdudu,ndugu zangu kumbe Tanzania tulioicha sisi siyo ya leo? Pongezi kwa serikali ya awamu ya 4 maana hizo zilizopita we acha tu zilinifanya mpaka NISEPE,hapa sisemi ya Baba wa taifa hapana mm naiheshimu sn serikali ya KAMBARAGE why coz yeye aliongoza katika wakati mgumu sn hasa pale mataifa fitina yalipo msusa na kumbana kiuchumi lakini kwa ujasili wake alituunganisha watanzania wote kuwa kitu kimoja pamoja na heka heka alizokumbana toka kwa mataifa papa,haki ya mungu najivunia kuwa mtanzania popote niwapo.

    ReplyDelete
  4. Mimi nashindwa kuelewa hii barabara ya magari yaendayo kasi iko katikati ya barabara mbili je hao abiria watakuwa unakatiza vp hizo barabara.....naona flyover ziko sehemu chache tu kituo kama cha magomeni nashindwa kuelewa kunavukwa vp wadau naomba mnielimishe kidogo

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 06, 2014

    michuzi ukichunguza sana, sehemu nyingi zinawekwa paving blocks kwenye mradi huu badala ya kupandwa miti, sijui wanamazingira wanasemaje kuhusu hilo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...