Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi,Ndg. Abdulrahman Kinana (wa pili kulia) akikabidhi funguo ya Pikipiki kwa mmoja wa Makatibu Kata katika Wilaya ya Kibaha Vijijini,wakati wa shunguli ya kukabidhi Pikipiki 13 kwa Makatibu Kata na Baiskeli 86 kwa Wenyeviti wa Matawi ya CCM yaliopo kwenye Wilaya hiyo,Vifaa hivyo vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini,Mh. Hamoud Abuu Jumaa (kulia).
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi,Ndg. Abdulrahman Kinana akikabidhi sehemu ya Baiskeli 86 kwa Mmoja wa Wenyeviti wa Matawi ya CCM katika Wilaya ya Kibaha Vijijini.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi,Ndg. Abdulrahman Kinana pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini,Mh. Hamoud Abuu Jumaa wakiwa wamepanda kwenye pikipiki hizo kwa kuzijaribu kama ziko vyema kwa matumizi ya Makatibu Kata waliokabidhiwa.

Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini,Mh. Hamoud Abuu Jumaa akiwahutubia wananchi wa Jimbo lake waliokuwa wamefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mtongani,kabla ya zoezi la kukabidhi Pikipiki 13 na Baiskeli 86 kwa watendaji wa CCM katika Jimbo hilo.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati wa kuwahutubia Wananchi wa Wilaya ya Kibaha Vijijini,Mkoani Pwani,ambapo amewataka Wananchi hao kutowaonea haya Watendaji wao iwapo watafanaya mambo ndivyo sivyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...