Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Ujenzi Bw. Mrtin Ntemo akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu maendeleo yaliyofikwa katika ujenzi wa barabara hapa nchini tangu Serikali ya  awamu ya nne ilipoingia madarakani . Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Frank Mvungi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Naomba mzee wa Libeneka usinibanie.

    Kwanza kabisa naanza kutoa hongera kwa juhudi zinazofanywa na serikali kujenga barabara nchini.

    Baada ya hongera nitoe ya moyoni.
    Tumechoshwa na ahadi za kujenga barabara za juu. Ni muda mrefu sasa tangu wimbo huu uimbwe na viongozi mbalimbali. Tunataka kuona vitendo. Nilitarajia kuwa mkutano wako ndungu mheshimiwa ungekuwa wa kutangaza kuanza ujenzi wa barabara za juu. Wataalamu wameisha eleza kuwa kwa siku tunapoteza si chini ya bilioni 5 (Rejea swali la Mhe. Mbatia kwenye Kikao cha Nane -Bungeni tarehe 12 Desemba 2013). Gharama za kujenga barabara ya juu ya Tazara kwa kadiri ya takwimu zenu ilikuwa bilioni 52.5/=. (The Guardian 1st November 2013) Sijui kama mheshimwa taarifa hizi unazo.

    Pili ninakerwa sana kuona hakuna juhudi zinazofanyika kuweka alama za barabarani zenye hadhi ya kimataifa. Wengi wanaondesha magari Dar es Salaam wanatumia uzoefu. Magari ni mengi alama zilizowekwa kuonesha mitaa mbalimbali na barabara za maeneo bado vile vialama vidogo vya pembeni. Kwa nini msiweke alama kubwa kama za kwenye mabango ambazo ndizo hutumika kwenye barabara kubwa? Bado tuko mbali ndugu mheshimwa. Si kwamba hatuna fedha la hasha, bali hatutaki kuamka na kufanya vitu kwa viwango na kwa weledi wa kimataifa. Utakuta mtu unaendesha gari unafika junction hujui hata uelekee wapi, hamna alama za uhakika. Someni ujumbe huu kwa makini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...