Basi la kampuni ya Japanese Express linalofanya safari zake kati ya Makete - Njombe likiwa limetumbukia mtoni mpakani mwa kata ya Lupalilo na tandala wilayani Makete mkoani Njombe, zaidi tazama picha zifuatazo hapa chini.
Katika ajali hii, abiria wameumia na kutibiwa katika hospitali ya Ikonda, hakuna abiria aliyefariki na kwa mujibu wa abiria waliokuwemo kwenye basi hilo wamesema chanzo cha ajali hiyo ni basi hilo kukutana na gari jingine kwenye daraja hili jembamba hivyo katika harakati za kumpisha mwenzake ili wasigongane uso kwa uso, ndipo basi hili lilipopoteza uelekeo na kutumbukia mtoni. Basi hilo lilikuwa likitokea Njombe kuja Makete mjini. Picha na Eddy Blog 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...