Liverpool leo wameheza  kandanda safi ingine kwa miaka kibao kwa kuichabanga  Manchester United 3-0 katka uwanja wao wa nyumbani wa  Trafford on Sunday,  huku mkongwe asiyezeeka  Steven Gerrard akitikisa nyavu mara mbili kwa njia ya penati na kulihamasisha Bwawa la Maini kwa mara ingine tena.
Kiungo huyo alipiga penati mbili za kufa mtu kuhakikisha vijana wa Brendan Rodgers wakiondoka na pointi tatu zote.
Luis Suarez aliongeza maumivi kwa Man U baada ya ‘chumba’ cha uhakika cha  Daniel Sturridge  kilipoguswa na kudondoka mbele yake,  ambapo raia huyo wa Uruguay hakufanya makosa alipochomeka kitu nyavuni mbele ya kipa wa Man U  David De Gea kumaliza kazi ya siku.

Ndio kusema Bwawa la Maini limechukua tena nafasi yake  pili (kuelekea ya kwanza) baada ya kuikopesha Manchester City kwa masaa kadhaa. Hadi sasa, kwa mujibu wa wataalamu wa soka,  hakuna sababu ya kulifanya Bwawa la Maini likose kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza kwa mara ya 20!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. LFC 4 LIFE! Kule Jamiiforum mbona kwikwi au ndio man united fans wamegomesha 3-0 mmezila. Pazi

    ReplyDelete
  2. nafikiri itakua mara ya 19 sio ya 20, ankal una wahi mbele mno,

    ReplyDelete
  3. Anfield FanMarch 17, 2014

    YOU WILL NEVER WALK ALONE!!! HAO NDO LIVERPOOL BWANA.....

    ReplyDelete
  4. HAHAHAHAH HOHOHOHOHHOKIKIKIKI LOLOLOLOOLO Y.N.W.A
    LA KUSEMA SINA

    ReplyDelete
  5. Wazee WA diving

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...