Meneja Kampeni wa Chama cha Deokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga, Alphonse Mawazo, akicheza ngoma ya jamii ya kimasai baada ya kufanya kampeni ya nyumba kwa nyumba kumnadi mgombea ubunge wa chama hicho, Grace Tendega Mvanda.
 Mgombea Ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika uchaguzi mdogo Jimbo la Kalenga, Grace Tendega Mvanda, akizungumza kuomba kura wakati chama hicho kilipofanya kampeni ya nyumba kwa nyumba na mtu kwa mtu katika Kijiji cha Mfyome
 Mgombea ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga, Bi. Grace Tendega Mvanda akishiriki chakula cha kimila pamoja na watu wa jamii ya kimasai katika Kijiji cha Mfyome jana asubuhi baada ya msafara wa mgombea huyo kufika kijijini hapo kufanya kampeni za nyumba kwa nyumba.
Mzee wa Mila wa Kimasai katika Kijiji cha Mfyome, Lioper Ilmuduji, akimpatia baraka mgombea ubunge wa CHADEMA katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga, Bi. Grace Tendega Mvanda, wakati chama hicho kilipofanya kampeni ya nyumba kwa nyumba kuomba kura kwa wananchi katika kijiji hicho.PICHA NA KURUGENZI YA HABARI CHADEMA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. wakati wa kuomba kura wagombea wote wanakuwa wanyenyekevu na kuonekana kama vile ni watu wazuri , wakishapata lao tu hawamjui nani wala nina , wanajisahau na mamilioni wanayolipwa na JK , hizi kazi za siasa husemwa ni za kizalendo na kujitolea lakini mbona zimebadilika kuwa za kikabaila na kujichotea fedha za wananchi ? nauliza tu naomba jibu. Nafikiri mafao na mishahara yao ikipunguzwa na kuwa ya chini kabisa ndipo tutapata wanasiasa wakweli na kuumwa na wananchi , ...ubepari ni unyama..grrrrrhoouwww

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...