HOTEL VICTORIA, ILIYO CHINI YA UONGOZI WA MDAU WA DIASPORA CHEF ISSA, IPO SHANGANI WEST MJINI MTWARA.  ILIFUNGULIWA RASMI TAREHE 14 FEB 2014 SIKU YA WAPENDANAO NA KUALIKA WATU ZAIDI YA 200. UNAWEZA KUPATA MAELEZO ZAIDI KWA http://www.hotelvictoria.me/ (JAPO BADO MATENGENEZONI)
 VYUMBA SAFI CHAKULA SAFI NA UKARIMU WA HALI YA JUU. HOTEL NAMBA MOJA MTWARA KWA BEI YA KAWAIDA.

Chef Issa (shati la draught) akiwa na wafanyakazi wake pamoja na wageni hotelini hapo. Yeye ni mmoja wa wadau wa Diaspora waliorejea nyumbani na kuwekeza. Globu ya Jamii inampa hongera Chef Issa kwa uamuzi huo, hasa wa kuchagua eneo nje ya Dar es salaam, na kukusudia kuleta huduma za kimataifa pamoja na kutoa ajira kwa wananchi. Hongera sana Chef Issa. Wewe ni M-Diaspora wa kuigwa!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Hongera sana kaka Issa, wewe ndo mfano wa kuigwa na wengine walioko huku nje. Hayo ndo tunayotaka sio kelele zisizo na tija. Hongera sana kwa kuleta maendeleo nyumbani.

    ReplyDelete
  2. Ewaaaaaaa! Haya ndio mambo tunayotaka kusikia. hapo Chef Issa mwanangu sio tu umepiga bao, bali pia umeonesha njia. Tumechoka na maelezo mareeeeeeefuuuu ya nini maana ya Diaspora..sijui nini... tunataka vitendo namna hii. Chef Issa nikija Ntwara (kwetu huko) lazima nitie timu hapo...

    ReplyDelete
  3. Anastahili pongezi kwa kuona fursa na kuifanyia kazi. Kila la Kheri ktk shughuli zako huko kwenye mji wa Korosho

    KK

    ReplyDelete
  4. Heko chef Issa. Hivi ndivyo Tz inavyotaka.Nenda nje ,ukota,kusanya nguvu lenga nyumbani.Hicho ni kitega uchumi kitakunufaisha wewe ,watoto na taifa letu kwa ujumla.Wakija wageni au watalii wakilala hapo watangiza fedha za kigeni utakula mpaka urambe,insurance kampani itapata,kodi ya mapato watapata na kama ukiwa na mpango huko ulikokuweko ukiitanga hoteli yako moja kwa moja wakifika uwanja wa ndege tu Taifa lapata. Kitendo cjako hicho ni maelezo tosha lakini kama una lolote watwike nalo madiaspora wasio na mapango zaidi ya kudai uraia pacha.Hongera tena.

    ReplyDelete
  5. watengeza na wauza vinyago pembeni wa hoteli yako na wao kutokana na initiatives zako na wao wataramba ramba,wavuvi wa pweza na samaki sasa kwa hoteli yako na wao mkwiji(pochi) wao utasheheni. Hongarea ,hongera sana ,nikuzindue kidogo wakija watalii wapikie pia mapishi ya kiafrika ndio utawaliza kabisaaaaa.

    ReplyDelete
  6. Sasa mnachogombea uraia pacha ni nini wakati mnaweza fanya investment home. Acheni kuwa na akili butu

    ReplyDelete
  7. Wadau #1 na #2 naona ubongo wenu umeganda. Siyo kila mtu anapenda kujitangaza kwamba anafanya iki au kile. Si asilia yetu wabongo. Ukijitangaza mtasema analinga kwa vilr katoka Ughaibuni. Pili, mtu anapojitangaza kama hivi si ndiyo kelele mnazozisema?! Nyie jamaa kweli wanafiki. Mngekaa na huo huo msimamo wenu kuwa jamaa Diaspola hawana faida. Ukweli ni lazima msome nyakati, mabadiliko ni lazima na usipotaka mabadiliko yatakubadilisha tu(msemo nimeutoa toka kwenye moja ya hotuba ya Kiongozi Malcom X-mawazo yaishi milele.)

    ReplyDelete
  8. Naona siku hizi kila siku imekuwa habari za uraia pacha. Naona jamaa wanaopinga hili wengi wao ni misukule, hawaelewi ishu, na wengi inaonyesha hawajawi hata kutoka nje' Jamani kusafiri nako ni elimu tosha(nahimiza uaptapo nafasi itumie). Upate matatizo au usipate safirini utakuwa umejifunza kitu. Naelewa wengi wanaweza wasipate fursa hiyo, lakini isiwe sababu ya kumbania mwenzio kwa bahati au juhudi aliyopata. Na iweleweke nimesema hivyo kwa sabau wengi wenu mnalazimisha kwa vile mtu yuko Ughaibuni lazima awekeze au afanye kitu fulani. Ukweli ni kwamba wengine maisha yao huko Ughaibuni haya jakaa sawa na labda maisha yao haya takaa sawa. Jamaa wanajimyima ili kuleta pesa kidogo nyumbani kwa upendo wao, ingawa watu wachache ndiyo wanafiki sasa hivi wanasema hawawataki. Wabongo tuache unafiki, fitina, ujinga usiolewaka kwani tuna vita kibao za kupambana nazo badala ya sisi kupambana wenyewe kwa wenyewe. Mfano, Wayahudi walikuwa hawana Taifa miaka mingi lakini wamekuwa matajiri haraka kuliko sisi kwa ushirikiano wao. Wala huwezi kusikia wanakanana kwa vile mmoja sijui yuko wapi wapi. Wabongo tuamke tuache polojo zisizo na msingi bali tuangalie ni nini bora kwetu, tutafika tu.

    ReplyDelete
  9. Point yako ya mwishoni ni shule. tatizo la sisi wenye ngozi nyeusi ni limukeni na wabinafsi. Mwafrika akipata tu hamjali mwenzake ni yeye na familia yake au na nyumba yake. Tupo huku nje hata ukutane na mwafrika njiani awe wa kenya or Tanzania ndo kwanza na jicho anageuza upande. Nafuu na Mkenya anaweza kukusalimu na kukusaidia ila sio baadhi ya wabongo sijumlishi maana kuna wengine wana roho nzuri. Mtu anajidai kasahau hata kiswahili au kisukuma, au sijui kinyakyusa kosa tu kuwa USA, or Ulaya. Tuache hayo ndo matokeo ya marumbano kwenye mitandao, tuige mifano ya wenzetu wayahudi na wavietnam huku America jinsi wanavyopendana. Na pia mtu akifanya kitu kizuri lazima apongezwe tusiwe na wivu, hata wewe jenga hostel or shule itangaze humu tutakusifu tu usijali.

    ReplyDelete
  10. Kuwekeza na kuchochea maendeleo na kuleta standard za ughaibuni nyumbani ni jambo zuri.

    ReplyDelete

  11. The one and only Tanzania world class chef Issa big up sana kiongozi wengi hawakujui uchakarikaji na bidii yako mimi nakufatiliaga sana kaza buti utafika mbali hata uamuzi wa kuwekeza mtwara umeona mbali sana. Hayo ndio matunda ya juhudi na pia umeonyesha mfano na thamani ya madiaspora. Tupeni uraia pata tuijenge nchi yetu kama India inavyothamini wahindi waliowekeza nje na wanaijenge hasa nchi yao hata wahindi waliopo hapa bongo wanathaminika sana kwao chuki haijengi.

    Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  12. CHEF ISSA YOUR THE STAR KEEP IT UP, MAJUNGU YAPO TU NA ULIYAJUA WEWE SONGA MBELE CHAPA KAZI DUH BONGE LA HOTEL, MTWARA INOGILE SIO

    ReplyDelete
  13. Kaka ukitaka hoteli hii ionekane baabkubwa weka mishikaki ya chamaki nchanga wachome kwenye nchale hahahahhahaaaaaaa duh bonge la kivutie kwa wazungu na watakula tu maana wenzetu wanapenda kujaribu kila kitu

    Mdau Netherland

    ReplyDelete
  14. BALAA IPO KWENYE KUMAINTAIN STANDARD JE NDIO UMEHAMIA MOJA KWA MOJA KAMA SIO DAH UTAUMIZA SANA KUPATA MENEJA BORA MAANA WABONGO MANENO MENGI UWEZO MDOGO SKY THE LIMIT CHEF KEEP UP THE SPIRITY. PIA MIMI NI FANY WAKO MKUBWA WA BLOG

    Dada yako Germany

    ReplyDelete
  15. Aisee kweli hii ni balaa nyie wadau hapo juu inamaana shida ni nini? huyu chef wa kimataifa kutangazwa mwana diaspora au kuitangaza biashara yake? soma vizuri muelewe kichwa cha habari alichopost michuzi hapo juu ni kwamba wana diaspora wameonekana hawana mchango wowote nyumbani aidha waliowengi wao hawapendi kuja kuwekeza nyumbani kwakutokubalika sasa huyu amejitosa nguvu zake, akili na mali kuirudisha nyumbani achene maneno ya kwejeli kwenye maendeleo pongezeni ndio tutafika msione wenzetu wanaendelea ni kwasababu wanaungana mkono.

    Mdau England

    ReplyDelete
  16. Hongera Chef Issa. Nakusahihisha kidogo ndugu Mdau hapo juu, wabongo hatupendani. Wengine tulioleta uungwana wetu wa kibongo huku 'nje' tumekomeshwa. sio kwambwa watu hatupendi kujuliana hali au kusaidiana, hapana. Mimi ni mmoja niliyekuwa nasimamia misingi ya 'undugu na upendo popote'. Mwenzenu yalinikuta niliemsaidia akakumbana na wageni (wa West Africa) na wenyeji wa nchi niliyopo wakaanza kuisumbua familia yangu, watoto wangu wakanyanyaswa nikatishiwa kushitakiwa polisi kwa ajili ya wema wangu. Mtu hana kibali cha kufanya kazi anasaidiwa apate chochote anageuza kibao. Mimi mambo ya oo msaidie fulani Hapana. Sasa hivi mimi na familia tunasonga mbele. Bora nimsaidie mtu aliyeko TZ lakini nje chungeni sana jamani kuna kugeuziwa kibao.

    ReplyDelete
  17. Wakati watu wanashangaa shangaa CHEF amesha CREATE JOBS ZAIDI YA 10.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...